Katika kuboresha na kuimarisha huduma ya maji mkoani Dodoma Mamlaka ya Maji
mkoani hapa (DUWASA) wameendelea kutanua wigo wa tenkonolijia kwa kutumia simu
za kisasa maarufu kama adroid kwa ajili ya kuhudumia wateja wao.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mawasiliano mamlaka ya
maji (DUWASA) mkoani hapa Bw. Sebastiani Warioba wakati akizungumza na kituo
hiki ofisini kwake, ambapo ameseama kuwa tenknolojia hiyo inasaidia mkupata
takwimu sahihi kutoka kwa mteja.
Aidha Bw. Warioba amewataka Wananchi mkoani hapa kutumia
mitandao ya maji taka vizuri kwa kutokutupa taka ngumu kwenye mitandao hiyo na
badala yake waitumie mitandao hiyo kwa kutupa taka laini ili kuzuia kuziba kwa
mitandao hiyo.
Mbali na hayo Bw. Warioba amefafanua kuwa kwa
kipindi hiki wakati serikali ikiendelea kuhamia mkoani hapa, serikali
imejipanga kugharamia ujenzi wa bwawa jipya la Falkwa kilometa 130 kutoka
Dodoma mjini kuelekea wilaya ya Chemba ambapo bwawa hilo litatumika kuhudumia
Na
Japhet Japhet Chanzo Dodoma
FM