
Akiongea na Benedict Ngelangela kutoka 98.4 dodoma fm radio kipindi Micharazo Time Jowzey amesema ni vyema waongozaji wa video wakawa wazalendo kwakuendelea kutumia location za Bongo kutengeneza video.
Ameongeza kwakusema waongozaji wengine wamekuwa wakisafiri kwenda nje kutokana na ushamba wa kwenda nje lakini si kweli kwamba wanafata vitu bora, na muda mwengine ni bora wakawaomba wasanii bajeti kubwa ambazo wanapeleka nje kwani ni vywema pesa zisitoke nje zibaki hapa hapa bongo na kukuza tasnia.
Aidha amesema akipewa bajeti ya kwenda nje kushoot video anaweza kwenda lakini nilazima iyo bajeti iwe yakutosha na mara nyingi wasanii hushindwa kufikia kiwango anachokihitaji ili akashoot nje ya Tanzania.