akiongea nakipindi cha micharazo time toka 98.4 dodoma fm radio Aslay amesema kwasasa anamipango mingi yakukuza muziki wake na amekuwa akiangalia ni jinsi gani ataweza kuufikisha muziki wake mbali hali ambayo inamuweka busy kila siku pamoja na kuangalia atawezaje kuachia wimbo autakao pendwa na kila mmoja.
Aslay ameongeza kwakusema kwasababu alianza muziki kwakusaidiwa na watu kwaio sio mbaya na yeye akaanzisha mfumo wakuwasaidia vijana wengine ambao wapo mtaani na wanavipaji lakini hawajapata nafasi ya kusikika kwa watu na ndio sababu ya kupata wazo lakuanzisha label Dingi Music.
Pamoja na hayo Aslay amesema kwenye label hiyo ya Dingi Musi mpaka sasa anawasanii wawili ambao walikuwa wakisimamiwa na mkubwa fella pia walikuwa wanaunda kundi la SALAM TMK ambalo kwasasa inasemekana limevunjika kutokana na wasanii kuhama kwani baadhi walichukuliwa na band ambayo inafanya muziki wa Bolingo.
Aslay amesema sababu za kuwachukua vijana hao nikutokana wanauwezo mkubwa kimuziki pia ni watu ambao wanaendana kisanaa.
Na Benedict Ngelangela