June26,2017
Chamwino Dodoma
Wakazi
katika Kata ya Mlowa Barabarani Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wanakabiliwa na
changamoto ya upungufu wa akiba ya chakula kutokana na kukosa mavuno ya kutosha
katika msimu wa kilimo mwaka 2017.
Diwani wa Kata
ya Mlowa barabarani Bw. Alan Nyahan Matheo ameyasema hayo wakati akizungumza na
kituo hiki baada ya kufika katika Kata hiyo na kujionea jinsi mazao ya chakula
yalivyoungua kutokana na kuchomwa na jua kali hali iliyosababisha wakazi hao
kukumbwa na uhaba wa chakula.
Bw.
Matheo amesema changamoto hiyo inatokana
na ukosefu wa mvua za kutosha katika msimu wa kilimo mwaka huu hatua
iliyochangia kuwepo kwa jua kali lililosababisha mazao ya chakula kukaushwa na
kuleta hasara kubwa kwa wakazi wa kata hiyo.
Aidha Bw.
Matheo amesema kutokana na changamoto hiyo iliyoikumba Kata ya Mlowa Barabarani
uongozi wa kata umelazimika kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya
akiba ya chakula kilichopo ikiwemo kuepuka upikaji wa pombe kwa kutumia mazao
ya nafaka.
Hata hivyo Bw.
Matheo amesema kwa kuzingatia kauli ya Serikali kuto kutoa chakula cha msaada
kwa wananchi wasio jishughulisha imeleta mwamko kwa wakazi wa Kata hiyo kujenga
nidhamu ya matumizi sahihi ya chakula cha akiba kilichopo ili kukabilana na
changamoto hiyo.
Na PiusJayunga
Chanzo: Dodoma Fm Radio