IRINGA MVUMI NI KATA NYINGINE INAYO KABILIWA NA CHANGAMOTO YA CHAKULA WILAYA CHAMWINO MKOANI DODOMA. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 27, 2017

IRINGA MVUMI NI KATA NYINGINE INAYO KABILIWA NA CHANGAMOTO YA CHAKULA WILAYA CHAMWINO MKOANI DODOMA.

                                              Chamwino Dodoma

Kata ya Iringa Mvumi Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa akiba ya chakula cha kutosha ili kukidhi mahitaji ya familia kwa wakazi wa Kata hiyo.

Image result for UHABA WA CHAKULA

Wakiongea na kituo hiki baadhi ya wakazi wa kata hiyo akiwemo Bw Bi. Lucy Mathias pamoja na Daniel Masanika wamesema hali hiyo inatokana  na kukosekana kwa mvua za kutosha hatua ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula.

Aidha wananchi hao wamesema kutokana na kujitokeza kwa hali hiyo imechangia kupanda kwa bei za mazao ambapo kwa sasa wananchi hao wanalazimika kununua debe la mahindi kwa kiasi cha shilingi elfu 22-25.

Diwani wa Kata hiyo Bw. Robert Chikole Mwaliko amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza sababu zilizo sababisha hali hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa mvua za kutosha hatua ambayo imechangia mazao kunyauka na hivyo kila mwananchi anapaswa kutumia vizuri akiba ya chakula kilichopo.

Wakati hayo yakijili, mapema hapo jana Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa akihutubia katika sherehe za Idd El Fitri Mkoani Kilimanjaro alisisitiza wafanyabiashara kuacha kuuza mazao ya chakula nje ya nchi na badala yake mazao hayo yauzwe katika Mikoa ambayo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa chakula.


Na PiusJayunga                                                            98.4 Dodoma fm radio

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages