LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU) SEHEMU YA 8 & 9 - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, September 1, 2016

LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU) SEHEMU YA 8 & 9

LOVE IS PATIENCE
SEHEMU YA NANE
MTUNZI; LULU HAMZA (LULU2HAMZA@GMAIL.COM)
  0656994884
 Displaying FB_IMG_1471413479200.jpg
Ilipoishia
Joseph akiwa anafikiria kutafuta kazi kwa ajili yake, na jinsi ya kumtafutia Prisca kazi
Endelea
Asubui na mapema Joseph alifika kwenye ofisi ya moja kati ya marafiki zake aliyeitwa William. “Kazi amepata vyeti vyake vizuri na nimependa kuwa anauzoefu na kazi” “Asante sana kaka yangu, basi saa nne atakuja hapa kwa ajili ya hayo maswali unayosema” “sawa haina shida”. Prisca alipata kazi kwenye  shirika jingine tena ila haikusaidia kitu maana bado mama Joseph alimfatilia hadi huko na kutoa fedha kwa mkurugenzi ili tu yule binti atolewe kazini na kweli walifanikiwa. Walichukua fedha za Prisca za miezi ya mwisho wakidai kuwa analipia pesa zilizopotea kazini kwa uzembe wake.
Prisca alimfata Joseph akiwa na huzuni sana “yaani kweli mama yako kanichomea moto vyeti vyangu, haya maisha nitakuwa mgeni wa nani mimi sasa” “tulia unieleze kakuchomea vyeti katika mazingira yapi?”. “Baada ya kuja kule ofisini alinifata nyumbani vizuri akaniomba vyeti vyangu na kusema atanisaidia kutafuta kazi. Na alisema kuwa anachukia sana baba yako anavyofanya kunitoa kazini” “ukampa vyeti?”. “Ndio nilimpa, ndio katoka nje ya nyumba kawasha moto” “usilie kiasi hicho basi usijari tutaangalia cha kufanya”. Alimpa moyo kidogo na kumuachia fedha ya matumizi japo na yeye hakupewa fedha tena na baba yake na kadi ya benk alinyanganywa.
“Mama kwanini lakini unafanya hivi? Haya umempotezea kazi yake kule pia mmeona msiishie hapo umemchomea vyeti vyake kweli mnaitaji nini?”  “uachane na yule binti mpango ya harusi na joyce ianze”. Joseph aliingia ndani akafikiria sana usiku mida ya saa tatu alitoka sebureni aliwakuta wazazi wake alikaa na yeye kwenye kochi. “Baba na mama nimekubali kumuacha Prisca” wote wakaacha kazi walizokuwa wanafanya na kumuangalia Joseph, mama yake aliachia tabasamu la furaha sana. “Hayo ndio maneno sasa mwanangu” “hivyo bwana inatakiwa uweunafikiria kama mwanaume bwana sio mambo uliyokuwa unafanya hapa” “ila nina ombi moja tu kabla sijaenda huko Tanga” “ombi gani mwanangu” baba yake alimuuliza.
“Naomba mumueke fedha Prisca kwenye akaunti yake ya benki, mnipe nikamueke na ikiwezekana mama ufatilie apate vyeti vyake. Kisha nitaondoka kwenda Tanga kuanza kusimamia kampuni na kufatilia harusi na Joyce”. “hilo halina shida basi mpaka kesho litakuwa limekamilika, ilo la vyeti mpaka kesho kutwa” “vikikamilika nitaondoka”. Kweli wazazi wa Joseph walifanya hivyo wakamtafutia Prisca kazi na kumuekea millioni tano kwenye akaunti yake.
Joseph alienda nyumbani kwa kina Prisca kumuaga “umebadilika sana mpenzi wangu, unielezei chochote imekuaje wazazi wamekubali kunitafutia kazi na kunirudishia fedha” “Prisca mpenzi wangu, niliongea nao wakaelewa wamejua jinsi gani nakupenda”. Prisca alicheka kwa furaha “mama amekuulizia amekukumbuka ila sasa ndio umemkosa ametoka” “nitamuona muda mwingine, Prisca nimekuja kukuaga nina safari kesho” “ya wapi na ya siku ngapi?” “Ya nchi za nje nadhani ya Zaidi ya miaka mitatu” “what!!? (nini!!?), safari ya miaka mitatu unaniambia leo hapa hivi?”. Joseph alivuta pumzi “siitaji unisubiri mimi mpaka nirudi, endelea tu na maisha yako nakuombea upate mume mzuri na familia yake ikupende” “mbona unanichanganya, unasafiri au unaachana na mimi?” “Naomba unisamehe Prisca”. Joseph alijitaidi machozi yasimtoke ila alijikuta ameshindwa kujizuia aliyafuta haraka kabla Prisca ajayaona “sitaki kuwa kunyume na wazazi wangu, nadhani hakuna haja ya sisi kuendelea kubishana na wazazi”.
“Lakini Joseph nitawezaje kuishi bila wewe unajua jinsi gani nakupenda kwanini unataka kufanya hivi sasa? Kama nilikosea nilivyomjibu mama yako kwa hasira naomba nisamehe sikujua kama atanirudishia vyeti vyangu” Prisca alikuwa analia tu. “Prisca haujakosea kokote ila nimeamua tu iwe hivyo sababu hatuwezi kuishi bila Baraka za wazazi tafadhali nielewe, ubaki salama Prisca kwaheri”. Joseph alitoka nje haraka mpaka lilipo gari lake na kuondoka gari kwa mwendo mkali. Huku Prisca akibaki amesimama pale pale analia alitoka hadi nje kumfata Joseph hakulikuta gari alijitaidi kulia taratibu ila uvumilivu ulimshinda akaanza kutoa sauti. “haa!! Kwanini mimi lakini jamani” alihii kizunguzungu na kuona giza alidondoka na kupoteza fahamu.
Asubui Joseph akiwa anaelekea uwanja wa ndege hapo Mbeya alipokea simu ya mama yake Prisca. “Halo baba huyu mwenzio kalazwa sasa hapa kaamka kaomba nikuite” “Prisca amelazwa?” alishituka ila alipogeuka alikutana na jicho kali la baba yake “twende ndege inakaribia kuondoka”. “haa! Sawa mama nitakuja kumuona sio muda” “sawa mwanangu kazi njema” “asante mama” aliingia na baba yake kwenye ndege kuelekea Tanga.
Prisca hakutaka kusubiri aliinuka na madripu yake mikononi alitaka kwenda ofisini kwa Joseph “amesema atakuja mwanangu kaa utulie mama wewe”.
Itandelea 


.........................................................................................................
LOVE IS PATIENCE
*SEHEMU YA TISA*
MTUNZI: LULU HAMZA (lulu2hamza@gmail.com)
Ilipoishia
Joseph akiwa anaelekea Tanga na baba yake, huku Prisca akiwa kazidiwa hospitalini mama yake alimuuguza**
Endelea
Joseph na baba yake walishuka Dar Es Salaam na baba yake na kuanza safari ya kuelekea tanga, haikuchukua masaa mengi sana mida ya saa kumi walikuwa tayari Lushoto. Walifikia kwenye nyumba ambayo baba yao aliijenga huko akiwa anaaanza maisha, muda wote huo Joseph hakuongea neno lolote japo baba yake alijitaidi kumsemesha. “Hii nyumba nimejenga kipindi hicho ndio naanza maisha nilivyokuwa mwalimu huku” “anhaaa nzuri, ya kisasa” “si nilirekebisha mwaka jana ndio maana hiko hivi” “anhaaa”. Siku ya kwanza ikaisha Wakiwa bize, ila siku ya pili Joseph akashindwa kabisa kufanya kazi.Usiku wote Joseph aliutumia kumuwaza mpenzi wake hakuweza kabisa kupata usingizi alitoka kwenye chumba alichokuwa amelala akiwa kavaa vizuri, aliingia chumbani kwa baba yake.
Baba yake aliyekuwa amelala fofofo hakusikia chochote, Joeph alibeba pesa zote za baba yake zilizokuwa kwenye mfuko wake akaondoka usiku huo wa saa tisa na kwenda stendi. Alipata magari makubwa ya mizigo yanayoelekea Dar “utakaa huko nyuma basi kwenye mizigo” “poa kaka cha msingi nifike tu hapo chalinze” “sawa”. Kweli alifika chalinze mapema mida ya saa kumi na mbili, pale alitafuta gari dogo linaloenda Mbeya “hapa gari la Mbeya mpaka saa mbili, ila kuna Noah ile inaenda Iringa alafu ukifika Iringa upande gari jingine” “sawa nipe hiyo siti moja iliyobaki”. Joseph hakuwa na mzigo wowote aliingia kwenye hiyo gari Ndogo safari ikaanza, yule dereva ni kama alijua kuna mtu anaharaka aliendesha gari kwa mwendo mkali.
“Hili gari langu leo yule kijana amekuombea sana, huwa sipakizi abiria kabisa” “asante sana mzee wangu, Mungu atakuzidishia” “inaonyesha unamatatizo sana, nini shida naweza kukusaidia?” “Hamna mambo tu ya familia kuna shida kidogo huko vijijini kwetu tunarudi kukamilisha” “vizuri sana, ndio ukubwa lakini kama unapesa hivi lazima ukawasikilize wazee”. Mida ya saa tano kasoro alikuwa amefika Iringa, waliagana na yule baba kisha alitafuta gari ndogo nyingine inayoelekea Mbeya. “nisaidieni bwana namuwai baba yangu yuko maututi anaitaji kuniona” “sawa basi panda” ilikuwa ni gari haina ya Land cruiz  safari ikaanza ya Mbeya.
Mida ya saa tisa alifika Mbeya akachukua tax mpaka nyumbani kwa kina Prisca, alifika getini akaona nyumba kama iko tofauti na hakukua na watu. “Samahani dada” “ndio kaka bila samahani” “wenye nyumba sijui umewaona au bado wako hospitali?” “hee!! Wewe ujui kama kuna msiba hapa? Wameenda kuzika sio muda sana” “kuzika? Nani kafariki?”.***
Huku baba Joseph alipoamka alimtafuta mtoto wake kila chumba akamkosa Ilibidi aeleke ofisini maana alishawaambia wafanyakazi hiyo ni siku ya wote kufika ili wapate maelekezo. “Huyu mtoto ukute karudi Mbeya sijui anaakili gani, nani alimwambia kuna mapenzi kwenye hii dunia anaacha kuangalia jinsi ya kupata fedha anaangaika na yule mwanamke kama mama yake”. Baba Joseph alichukua sana ila hakuwa na la kufanya kwa siku hiyo na simu ya mtoto wake ilikuwa haipatikani siku nzima. “Mama Joseph nataka uangalie kama huyo mtoto kaja huko” “mmmh! Atakuwa amekuja kama hayupo huko muda wote, na sijui akifika huku itakuwaje?” “Kwanini?” “Yule binti amefariki, Prisca”***
Joseph kusikia jina la Prisca aliishiwa nguvu akabaki anamuangalia yule dada aliyempa taarifa, “haiwezekani” aliingia kwenye gari akaliondoa kwa mwendo mkali mpaka kwenye makabuli aliyoambiwa wameenda. Vumbi lililoletwa na gari la Joseph likafanya watu wote pale makaburini wageuke kumuangalia, Joseph hakujali alishuka mbio mpaka lilipo Jeneza. Alisimama kwanza kwa muda kama hataki kuangalia nani yupo ndani alimuangalia mama Prisca na wadogo zake waliokuwa wameshikwa na watu. “Naomba nimuone” aliongea ila safari hii alipiga hatua taratibu na kwa uwoga mwili wake wote ulitetemeka akajitaidi kuvuta pumzi aliyoona inaisha. Alipoona uso wa Prisca uliorembwa na pamba kila sehemu n Macho yaliyofunikwa alipiga magoti taratibu pembeni ya lile jeneza “Prisca, Prisca mama, nimerudi mpenzi wangu naomba unisamehe. Naomba uamke mpenzi wangu sitoondoka tena nakuahidi mpenzi wangu”. Joseph Alianza kulia kama mtoto wa kike sasa jambo lililofanya waliokuwa wamenyamaza waanze msiba upya, Masikini Prisca wake hakuamka tena wala hakuweza kuitikia pale ambapo Joseph alimuita kwa maneno mazuri.
Prisca alizikwa wanaume wenye nguvu walimshika Joseph aliyeteka kuingia kaburini. Joseph alirudishwa na gari lake hadi kwao “asante sana kaka kwa kumleta” “sawa mama mimi naenda” Josseph hakuongea na mama yake aliingia ndani kwake akafunga mlango. Alilia huko ndani kama mtoto ikabidi mama yake na Josephine watafute funguo za mlango wafungue “au mlango uvunjwe mama fungue zile azionekani?” “Sasa na nyie mliweka wapi lakini? Asije akajiua mwanangu jamani muite mlinzi avunje mlango uwii”. Mama Joseph alichanganyikiwa akazunguka nyumba nzima akisubiri kitasa kivunjwe ili akamuangalie mtoto wake.
“Nusu ya moyo wangu imechukuliwa, nahisi kama namkufuru Mungu kwenye hii Dunia. Kwanini niliondoka ningebaki asingekufa, nimemuua mwanamke wa maisha yangu mimi mwenyewe bora na mimi nife tu ijulikane moja ”. Kwa mbali uliweza kusikika wimbo uliokisindikiza kilio cha Joseph huko ndani. “A RED RIVER OF SCREAMS, UNDERNEATH. TEARS IN MY EYES….. UNDERNEATH DEPTH OF MY SIN, LOOK AT ME NOW..” . Joseph alijuta na kuona kama yeye ndiye aliyemuua mpenzi wake .
Usikose kujua maamuzi hatayo yafanya Joseph baada ya hapo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages