LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU) SEHEMU YA TATU. - NGELANGELA NEWS

Post Top Ad

Saturday, August 20, 2016

demo-image

LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU) SEHEMU YA TATU.

Responsive Ads Here
LOVE IS PATIENCE
MTUNZI: LULU HAMZA
SEHEMU YA NNE
?ui=2&ik=0c85e109a2&view=fimg&th=156972b055ed14a4&attid=0
ILIPOISHIA
Adventina akiwa kafahuru vizuri kidato cha sita, ila alipoteza kabisa heshima kwa dada yake
ENDELEA
hatimaye Adventina alifanikiwa kwenda chuo katika jiji la Dar Es Salaam, alipoenda huko hakuwa tena na mawasiliano na nyumbani kwao. Zilisikika tu hadithi kuwa amekuwa waziri wa chuo na amekua na fedha kushindwa wanafunzi wote pale chuo. Uzuri wake ulimsaidia Zaidi kupata fedha za kumtosha, fedha zikamfanya azidi kuwa mrembo Zaidi kushindwa alipokuwa kwao.
Janeth alipambana na kufanikiwa kumuamisha mama yake ule mtaa waliamia mtaa wa kstaarabu kidogo na mgahawa ukawa sehemu nzuri na wa kisasa. Walipanga vyumba viwili na kwa muda wote huo Janeth alikuwa na miaka ishirini na tatu, japo Alifanya kazi nyingi ila bado uzuri wake ulionekana machoni kwa watu. Alikuwa ni msichana mwenye weusi wa mzuri wa kuteleza, alikuwa na mwili mwembamba ulioumbika vizuri. Alijaliwa shepu nzuri na miguu ilyojaa vizuri. Acha vyote sura yake nzuri ndio iliwashitua wengi hasa pale alipotabaamu alimzidi kuimbamba sura yake kwa dimpo lake moja kwenye shavu.
Siku moja Janeth akiwa kwenye mgahawa wake mpya waliingia watu waliovaa vizuri na nguo zao zilionyesha ni watu wa heshima. walikuwa wakina dada wawili na wakaka watatu, Mmoja kati ya wale wasichana alikuwa amesoma shule moja (sekondari)na Janeth alijulikana kama Hosiana. Alikuwa ndiye rafiki yake kipenzi Janeth Wakiwa shuleni mpaka watu wengine walijua ni ndugu, ila Hosiana alikuja kuamia Mbeya baada tu ya kumaliza kidato cha nne.
Hosiana: msaidizi, huyu ndio huyo dada niliyekwambia anapika vyakula vizuri na anaweza kuwa
              Anatuletea chakula pale ofisini. Kuondoka usumbufu wa kufata chakula. Anaitwa Janeth
             Ni mwenyeji wa hili eneo sana.
Msaidizi (mkaka): nashukuru kukufahamu Janeth, kweli naona hata mazingira hapa ni mazuri na
                               yana furahisha. Chakula je kipo  Hivyo ?
Janeth: ndio baba chakula ni kitamu sana nakuakikishia hamuwezi kujuta kunichukua hapa. Wot
             e lazima mpate afya. (wote walicheka pale).
Mdada: Mimi naona tumchukue huyu huyu dada sababu ya usafi tu kwanza na ujirani na
             Kampuni yetu mpya.
    Waliongea nae kidogo kisha walipata chai na kuondoka, ila hosiana alibaki nyuma. “hee!! Nashukuru sana rafiki yangu sijui nikwambie vipi” “usijari Janeth maisha ni kusaidiana, hii kampuni ndio imeanza wanachapisha vitabu, magazeti, na pia wanatengeneza karatasi, madaftari na vingine” “anhaaa hee labda na mimi nitakuwa tajiri sasa” “hahaha usinichekeshe rafiki yangu”. Janeth alifurahi sana maana uchumi ulikuwa umepanda sana na alipata wakati mgumu kununua dawa kwa ajili ya mama yake.
    Hatimaye jumatatu ilifika Janeth Alianza kupeleka chai asubuhi na chakula cha mchana kwenye hiyo kampuni mpya. Ilikuwa ni kampuni ya kisasa sana kwa eneo lile, ilikuwa na ghorofa mbili na ilizungukwa na ukuta mkubwa sana. Wafanyakazi walimpenda Janeth na walifurahia sana chakula chake, jambo lililofanya wanaume ambao awajaoa wamuagize na vyakula vya jioni. Alikuwa msafi na vyombo vyake viling’aa sana,wanaume wa ofisi hile wakaishia tu kummezea mate. “mmh Hosiana rafiki yangu huyu boss wenu anashida gani?” “yaa achana naye sijui ananini hata kampuni ile tuliyotolewa kule Mbeya walikuwa wanamuogopa” “Hafai kuwa hivi”.
    Huyu waliyemuongelea hapo juu alikuwa ni boss wa kampuni hiyo, alikuwa ni kijana mdogo wa miaka ishirini na sita. Alijulikana kwa jina kama Joseph Japheth alikuwa ni mtoto wa kwanza akifatiwa na mdogo wake wa kike aliyeitwa Josephine. Joseph alikuwa ni kijana mzuri sana mwenye kila sifa ya kuitwa mwanaume na kumvutia kila msichana, wafanyakazi wa kike na hata wanawake wa nje walivutiwa naye. Ila tabia yake ya ukali na kugombeza watu kwa kosa dogo kulifanya watu wasimpende tena na kupoteza hata uzuri wake.
USIKOSE KUJUA NINI KILIMPATA JOSEPH.NA MAISHA YAKE KWA UJUMLA

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *