LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU)
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI; LULU HAMZA (lulu2hamza@gmail.com)
Katikati ya mji wa Lushoto, mitaa ya uswahilini sana anaonekana mama mwenye maisha ya hali ya chini. Ni mama wa makamu tu mwenye miaka kama thelathini na nne kwa kumuangalia ila ugumu wa maisha unafanya aonekana kama mtu wa miaka arobaini na tano na kuendelea.Mama huyu alikuwa na watoto warembo wawili wa kwanza aliitwa Janeth na wapili aliitwa Adventina. Mume wake alifariki ghafla kwa mshtuko uliodaiwa uliletwa baada ya mwanaume huyu kufukuzwa kazi, na nyumba zake mbili na gari kupigwa mnada. Alifariki na kumuachia mke wake watoto wadogo Janeth alikuwa la pili na Adventina alikuwa chekechea. Mama yao anaamua kwenda kupanga vyumba viwili ila baadae maisha yanazidi kuwa magumu anaamia mitaa ya uswahilini iliyoitwa Kitanzini. Anapanga chumba kimoja ambacho alilipia elfu ishirini kwa mwezi.
Kitanzini ni mtaa uliokuwa na kelele za kila aina miziki, vigodoro na kila siku walipiga mwizi. Vichochoro vilikuwa vingi na kila sehemu kulikuwa na mtaro wa maji machafu. Mama Janeth alitafuta kibanda akaamua kuanza kujishughulisha na kupika, biashara yake mwanzoni ilikuwa ngumu ila baadae watu walimzoea na akawa na wateja wa kutosha. Watoto zake walisoma vizuri na kuvaa vizuri alijitaidi wapate kila kitu ili tu wasijisikie vibaya Wakiwa na wenzao.
Janeth alifanikiwa kumaliza kidato cha nne na kufahuru vizuri kwa daraja la pili. Alichaguliwa shule ya kazima iliyokuwa mkoani tabora, “sasa mwanangu utaendaje mbali hivyo, nauli ya huko ni elfu sabini bado ada na michango ni laki na nusu. Aya sijakushonea sare za shule na kukupa fedha ya matumizi” “sijui sasa kama utapata fedha nitaenda kama ukikosa basi nitasubiri hadi mwakani” “usijari lakini ngoja nione”.
Janeth alikosa fedha ya kupelekewa shule ikabidi huo mwaka abaki nyumbani. Aliamua kufanya kazi ambayo aliamini akihifadhi fedha zake anaweza kupata ada ya kulipia shule na ela ya matumizi pia. Alikuwa akitengeneza juice na kuzungusha kwa madereva wa pikipiki (boda boda) na kwenye maduka ya watu. “ufiche hiyo faida itakusaidia mwakani kwenda shule” “sawa mama” “ngoja na mdogo wako amalize kidato hichi cha pili michango ipungue maana mitihani kila siku”. “hizi shule zetu za serikali bwana”.
Janeth alikutana na vikwanzo vingi sana huko barabarani alikotembeza juice, hasa vikwanzo toka kwa wanaume wajinga ambao muda wao mwingi wanatumia kuwaza ngono. “janeth leo nataka kununua juice na muuzaji wa juice” “embu usinishike bwana, kama unataka juice lete kopo nakuwekea” “mimi sitaki juice sasa nakutaka wewe, nakupa elfu ishirini tunalala nusu saa unaondoka na ndoo zako” “embu achana na mimi unadhani mimi ni kama hao malaya uliowazoea”. Janeth alibeba ndoo yake ya juice akaondoka msimamo wake ulimsaidia sana kuepuka vishawishi pia maneno ya mama yake yalimtia moyo kila alipokutana na watu wa aina hiyo.
“Adventina mdogo wangu ukazane kusoma haya makundi ya marafiki wa ajabu hayotokufikisha sehemu unaiona hali ya hapa kwetu lakini” “mimi nasoma dada nyie tu amniamini” “haya mama”.
Chumba chao kimoja kilijaa hadi mlangoni, kitanda cha tano kwa nne, kochi moja, kabati dogo la vyombo na Tv. Adventina alimaliza kidato cha pili na yeye akawa nyumbani, muda wake mwingi alitumia kwenda kutembea kwa marafiki zake ambao kwao walikuwa na maisha mazuri. Sababu alikuwa mtoto kipenzi wa mama yake walimuacha afanye vile alivyopenda.
Ikiwa imebaki miezi minne ili Janeth aende shule, alifanikiwa kununua maitaji yote muhimu kwa ajili ya shule. Ikiwepo madaftari, shati la shule, sweta na vingine vingi, mama yake alikuwa kamuombea uamisho wa shule ya jirani ambayo ilikuwa ni shule ya kutwa hivyo angelala tu nyumbani. Siku hiyo waliamka asubuhi hali ya Adventina ilikuwa sio nzuri kiafya “Janeth embu mpeleke mdogo wako hospitali, japo sina fedha leo ila tumia yako nitakuja kukupa” . “Sawa mama haina shida, jiandae twende Adventina” “sawa dada”/
Waliingia hospitali ambako walitumia fedha nyingi kupumima vipimo vyote baada ya kuona hakuna ugonjwa unaoonekana na mtu yupo hoi kabisa. “Ngoja nimuandikishie kipimo cha mwisho sasa” “sawa” walienda kuupima “tushatumia elfu kumi sijui kama ela itatosha hata dawa itabidi nikaongeze fedha kama watasema fedha nyingi” “sawa dada”. Walirudi kwa daktari kusomewa majibu ya kipimo cha mwisho “huyu mdogo wako inaonyesha anamimba.” Janeth alishituka akabaki anamuangalia tu Adventina, ila Adventina alibaki anaangalia chini. Walitoka pale hospitali bila hata kuongeleshana kila mtu alikuwa kimya “dada nisaidie fedha nikatoe” Janeth alimgeukia mdogo wake bila kumjibu akamuangalia na kutikisa kichwa kwa kusikitika. “ulivyokuwa unapata ulijipanga kuua kiumbe cha watu?” “sio hivyo bwana hata wewe unaweza kupata kwa bahati mbaya” “Usitoe hiyo mimba bwana ni dhambi kubwa kabisa” “sasa unadhani mama ataipokeaje hii taarifa atakufa bure kwa mshituko najua nimekosea ila sitaki kumfanya mama yangu apoteze amani yake”.
Janeth alimuangalia mdogo wake macho yake ya upole yalikuwa yamekuwa mekundu akajizuia kulia, maana alijitaidi sana kila siku kumwambia mdogo wake kuhusu ugumu wa maisha. “sina fedha ya kukupa, ela zangu zote mama amechukua kunihifadhia hapa nilibaki na hii fedha aliniachia ni nunue vitu nguo za ndani” “sasa hiyo elfu kumi haitoshi, daktari kasema elfu hamsini” “muombe huyo aliyekupa mimba” “sawa ngoja nimfate tutakutana nyumbani baadae” “ujitaidi uwai”.
ITAENDELEA...........