LOVE IS PATIENCE
MTUNZI; LULU HAMZA (lulu2hamza@gmail.com)
SEHEMU YA TATU.
ILIPOISHIA
Mama Janeth akiwa karuhusiwa na Janeth alirudi nyumbani ili kumwandalia chakula mdogo wake. Aliwaza vitu vingi sana juu ya maisha yake akahisi ndoto zake zote zinaishia pale.
ENDELEA
Maisha yakabadilika na kuwa magumu Zaidi, Janeth akawa ndio mama wa familia hiyo. Mama yake hakuweza tena kazi ngumu baada ya kupooza upande wake wa kushoto wote. Janeth aliendeleza mgahawa wa mama yake alijitaidi sana kufanya biashara na alipata faida ila yote iliishia kununua dawa za mama yake na kumuandalia mdogo wake vitu vya mtoto. Advetina alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike aliyeitwa jina la bibi yake “Hellen” wote wakafurahi sana. “nimemletea mtoto kitanda chake ili asilalie mashuka yetu haya” “hee asante sana dada yangu, shingapi kitanda kizuri hivi?” “wamenipunguzia hadi elfu thelathini” “mama kitanda cha mjukuu wako”.
Janeth aliilisha familia na kulipa kodi zote pia kuakikisha mtoto anapata vitu vyote vya msingi. Alikuwa na wateja wengi sana kwenye mgahawa wake na watu wengi walimpenda kwa ajili ya usafi wa vyombo vyake na mazingira ya pale. “Adventina ujitaidi kumnyonyesha mtoto mwakani urudi shule umefahuru kidato cha pili vizuri” “sawa dada na mtoto atabaki vipi?” “nitakuwa naenda naye na mama anaonyeha kuwa na maendeleo mazuri” “sawa dada”. Usiku wote Wakiwa wamelala Janeth alitumia huo muda kuwaza afanye nini kuiinua familia yake elimu alishaikosa alijikuta analia tu.
Kila asubuhi Janeth alionyesha kuwa na furaha ila alikuwa na mawazo sana, Alifanya kazi kwa bidii sana. Kweli baada ya mwaka. Adventina alirudi shuleni na mtoto alibaki nyumbani na mama yao ambaye alikuwa akifanya kazi pale nyumbani hali yake kiafya ilikuwa nzuri. “ila mama ungepumzika bado haujapona sana” “hamna kukaanga tu miogo na viazi hapa nyumbani haina shida” “na huo mkaa unaotaka kuanza kuuza?” “Ila lazima nikusaidie mwanangu, ukinipangia mkaa kwenye makopo asubuhi basi mimi nawambia wajimiminie na Adventina atatusaidia” “haya”. Mama Janeth aliuza miogo na viazi vya kukaranga na mkaa kwenye makopo.
Miaka miwili mbele Adventina alimaliza kidato cha nne, mtoto wake alikuwa na miaka mitatu “sasa hii rikizo kuna mtu nimemuagiza vitenge na vikoi nataka utembeze mtaani” “haa dada Janeth mimi siwezi kuzunguka mitaani”. “Basi ukauze mgahawa mimi nifanye hiyo biashara maana mkaa utaki kushika pia sasa unaweza nini?” “Labda mnifungulie duka sasa kweli hata nikionekana na rafiki zangu..” “mtoto wako anatakiwa kwenda shule unategemea dada yako akulipie wewe ada mwakani na mtoto wako ampeleke shule au?” “Sio hivyo mama” “ila nini?”. Janeth alihisi hasira alitoka nje na kuendelea na kazi zake mama yake alimfata “basi unipe niwe natembeza vikoi jioni?” “Mama unaona hali yako kila siku tunaangaika hospitali, usijari nimejua cha kufanya”.
Janeth kila jumapili alifunga mgahawa, alipotoka kanisani alipita nyumba za watu na kuwauzia wadada na wamama vitenge, sidiria na chupi. Aligombana sana na mdogo wake “una nini lakini Adventina kila kitu unamuachia dada yako, na mtoto wako pia unataka uangaliziwe na mtu hupo hapa nyumbani” “kwani kuna shida gani mtoto wangu si wake pia”. “alafu wewe nisikusikie ukiongea ujinga huo huyu mtoto ulitafuta na dada yako si ujinga wako ndio umesababisha?” “Mama na wewe unaona kama huyo mtoto wako ndio malaika sababu tu yeye analeta fedha za matumizi hapa nyumbani unataka na mimi ni mnyenyeke….”. Kabla ajaendelea kuongea mama yake alimrushia kibao cha nguvu usoni kabla mama yake ajainua tena mkono alidondoka “hee!! Mama”. Alianza kumpepelea na kufungua mlango hewa iingie ndani ya nusu saa Janeth aliingia na Hellen akiwa mgongoni kwake “mama anaumwa mbona kapoa hivyo?” “Anaumwa ndio anajijua mgonjwa alafu anataka kukalipa”.
Janeth alimshusha Hellen akamsogelea mama yake “umekula mama?” “Bado” “umepika nini jioni hii Adventina” “nipike nini na hamna cha kupika” “mbona niliacha maharage” “sasa hayo maharage kila siku khaa mimi nimechoka kuchemsha maharage kila siku tununue chipsi tule” “na mtoto wako atakula nini?” “Hizo hizo chipsi ale nini sassa”. Janeth alienda gengeni jioni hiyo akanunua mboga za majani, nyanya chungu na unga wa ugali akiwa anarudi alishituka watu wamejaa barabarani “masikini mtoto wa watu na boda boda imekimbia”. Janeth alijikuta amedondosha mfuko wake chini baada ya kumuona Hellen pale chini alikimbia kumuinua alikuwa kajaa damu.
Hellen alitoka baada ya kuona mama yake mkubwa anaondoka na Adventina hakujali hata kusema amrudishe ndani alijua mtaa wao boda boda zilikuwa haziendeshwi na watu wastaarabu hata kidogo. Masikini Janeth alimbeba mtoto walipanda kwenye bodaboda iliyowakimbiza hospitali walipokelewa kwa haraka na mtoto kuingizwa wodini. “Tulia hapa dada tutakuita” “sawa” mama yake na Adventina Waliingia hospitali baada ya muda pia “anaendeleaje mtoto?” “wamesema nisubiri watatuita”. Janeth alimuangalia mdogo wake kwa hasira sana alijitaidi asionge kitu daktari alitoka aliongea maneno mengi ila neno moja lilipita kwenye moyo wa Janeth kama msumeno wenye meno pande zote mbili. “Hivyo basi mtoto amefariki”.
Yule mtoto alikuwa ni kama wa Janeth na yeye ndiye aliumia sana kushindwa maelezo, alikuwa kamzoea sana na hakuzani kama anaweza kafariki akiwa bado mdogo vile alikuwa anamuwazia mambo mengi sana. Baada ya kumaliza kuzika Janeth alipumzika kidogo kabla ajarudi kwenye biashara “wewe umesababisha kifo cha mwanangu, mtoto anakufata hata kumshika mkono ukaona kazi” “sihitaji maneno Adventina tafadhali sana mdogo wangu” “haya si umefurahi kafariki ili ukazane na biashara zako yaani mnaona kunisaidia kumlea mwanangu ilikuwa kazi kweli kwenu”. Janeth aliinuka akatoka nje
Adventina aliingia kidato cha tano na alilipiwa na dada yake, japo kuwa hakumuheshimu kabisa dada yake aliweza hadi kumuita dada yake kahaba. Akidai kuwa dada yake alijiuza ili kupata pesa zile zote “utajilipia wewe sasa huko chuo si unaringa hii form six umemaliza” “nitajilipia kwanza nina mkopo wa kutosha usinitishe hauna jipya” “asante sana mama, leo mimi si sina maana”.
&&& usikose kujua hatima ya wadada hawa wawili baada ya Adventina kwenda chuoni.
Itaendelea