POLISI AUWAWA KWA KUKATWA MAPANGA, CHANG'OMBE DODOMA - NGELANGELA NEWS

Post Top Ad

Wednesday, February 4, 2015

demo-image

POLISI AUWAWA KWA KUKATWA MAPANGA, CHANG'OMBE DODOMA

Responsive Ads Here
Huku matukio ya kuwadhuru askari polisi yakijitokeza siku za nyuma, lingine limetokea leo siku ya juma tano tar 4 mwezi wa 2,2015 saa 5 kamili asubuhi mkoani dodoma kata ya chang'ombe.


ajali
kamanda wa polisi dodoma Misime D.A


www.ngelangelanews.blogspot.com

STORY KAMILI.
Chanzo cha kuuwawa polisi huyo aliyekuwa akifahamika kwa jina la kwa jina la JOSEPH  ISACK SWAI namba G.7168 N kwamba alipigiwa simu na mtendaji wa mtaa wa chang'ombe juu hapa dodoma mjini akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa OLIVER D/O BALTAZARI miaka 52,(chaga) mkazi wa chang'ombe juu, kuwa kijana wake aitwaye TISI S/O SIRILI MALYA anamtesa mtoto wake mdogo wa miezi nane aitwaye VALERIAN S/O TISI MALYA na anahisi labda aneshanuua kwani mtoto huyo halii tena.

Alichofanya mtendaji huyo ni kumpigia askari huyo simu naye akaenda hadi ofisi ya huyo mtendaji wwa mtaa. Waliongozana wote wakiwa pamoja na kijana mmoja hadi anakoishi huyo TISI S/O MALYA. walipofika askari aligonga mlango na akajitambulisha kuwa yeye ni askari hivyo atoke nje.
Alichokifanya mtuhumiwa huyo ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi nane kwa mkono miguu juu kichwa chini na kutaka kumkata  kwa panga na kusema namkata shingo sitaki kuona mtu.

Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo na alipomrukia mtuhumiwa kwa bahati mbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari huyo na akadondoka chini kutokana jeraha kubwa alilomsababibishia.,
Hata hivyo mtuhumiwa huyo aliendelea kumkatakata na mtendaji na kijana waliyekuwa naye ambaye ni mratibu wa watoto wanaoishi kwenye katika mazingizrz magumu iliwabidi kukimbia huku wakipiga kelele kuomba msaada.

Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyma alikimbia huku nguo zake zakiwa zimetapakaa damu akiwa na panga mkononi.

Askari huyo muda mfupi kabla ya tukio hilo alikuwa ametokea katika kituo cha rediocha Dodoma fm kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi.(albino)tunapoelekea kipindi hiki cha uchaguzi kwani mbali na kazi anazofanya moja wapo ni kushiriki katika vipindi vya elimu ya polisi jamii hapa mkoani dodoma.

Msako bado unaendelea ili kuwez kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu aliyesababisha kifo cha askari huyo wakati alipojitolea maisha ili kumwoka huyo mtoto mdogo.

jeshi la polisi linzidi kuomba msaada wa wananchi popotte pale watakapomuona TISI MALYA miaka 29, mchaga ambaye ni maji ya kunde,mwembamba,siyo mrefu sana saizi ya kati alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na tshirt rangi ya dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu ili aweze kufikishwa mahakamni.
source kamanda wa polisi dodoma

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *