hivi karibuni aliwaacha baadhi ya mashabiki wake midomo wazi na kuwapatia maswali yasiyo na majibu baada ya kupost picha iliyo na utata kwenye ukurasa wake wa facebook.
jaco beat alipost picha ikumwonesha akiwa na dada ambae inasemekani ni mkurugenzi wa studio za coco records zinazo patikana barabara ya sita mkoani dodoma ikiwaonyesha wakiwa katika mapozi ya kukabidhiana funguo ya gari.
![]() |
jaco beat akiwa na mkurugenzi wa coco records |
baada ya kuona watu wapo njia panda ndipo mtandao huu kwa kushirikiana na kipindi cha Micharazo time toka 98.4 dodoma fm radio kikiongozwa na jizzle volt pamoja na Benedict Ngelangela kuamua kumtafuta jaco beat mwenyewe kuweza kujibu maswali hayo.
akifunguka kupitia micharazo time jaco beatz alipoulizwa juu ya yeye kukabidhiowa gari hakuwa na ksema zaidi alionyeshwa kufurahishwa na swali hilo na kuishia kucheka.
alipoulizwa kuwa ni kweli ngebe imempatia gari na yule aliyekuwa anamkabidhi gari ni nani akiwa anaheka alisema hayupo tayarai kuzungumzia swala hilo kwanisio muda wake huu ila muda ukifika atawajuza watu wote.
@@@ siwezi sema lolote kwani muda haujafikia kuliweka wazi swali hilo we ngelangela kwani mtu akinunua gari mtaani kwenu lazima umtangaze? we subiri nikutane nawe barabara then nikupe lift nikuwaishe ofisini tu we subiri sitaweza kuongea kwasasa ila nitaongea kwa vitendo we subiri kuona@@@
aidha jaco beat alipost picha ikimounyesha akiwa anasaini mkataba ambao bado haijajulikana mpaka sasa ni nini kilikuwa kinaendelea na hakuwa tayarari kulisemea.
