DODOMA FM RADIO KWA KUSHIRIKIANA NA WADUA KUTOA MISAADA KITUO CHA KINAMAMA CHIKANDE SIKU YA VALENTINE DAY. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, February 13, 2015

DODOMA FM RADIO KWA KUSHIRIKIANA NA WADUA KUTOA MISAADA KITUO CHA KINAMAMA CHIKANDE SIKU YA VALENTINE DAY.

 

kituo cha radio mkoani dodoma, dodoma fm radio kimepanga kuonyesha upendo kwa wakazi wa dodoma siku ya wapendanao ambayo ni juma mosi ya tarehe 14 katika kituo cha kuwasaidia wakina mama wenye matatizo mbalimbali hususani katika maswala ya uzazi.

akizungumza na mtandao huu meneja wa kituo hicho ZANIA MIRAJI amesema wameamua kufanya hivyo kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali ili kuweza kuweka ukaribu watu pamoja na kuwafarijiana pia.
aidha ameongeza na kusema kampeni hii ni kamapeni endelevu na ilianza mwaka 2013 na kwa mwaka huo walitembelea magereza ya isanga na itakuwa endelevu kwa kila mwaka na imepewa jina la ONYESHA UPENDO.
Amemalizia na kusema anawashukuru baadhi ya watu ambao tayari wamesha toa michango yao kama nguo, viatu pesa.nk lakini bado wanakaribisha kila mtu kuongozananao kwenye matembezi hayo ya kuelekea chikande kwani yataanza mida ya saa nne asubuhi wakitokea katika ofisi za dodoma fm radio.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages