WYSE1 AWATUPA WAPENZI WAKE WA DODOMA/ NINA MPENZI MPYA MAARUFU NCHI NZIMA ANAFAHAMIKA - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, August 22, 2018

WYSE1 AWATUPA WAPENZI WAKE WA DODOMA/ NINA MPENZI MPYA MAARUFU NCHI NZIMA ANAFAHAMIKA


Msanii wa Muziki Abdul Aziz kwa jina la sanaa anafahamika kama WYSE1 ambaye anafanya kazi chini ya usimamizi wa msanii mwenzake Ben Pol amefunguka juu ya ujio wa nyimbo zake mpya pamoja na kurudia nyimbo za wasanii wengine.
Akizungumza na kipindi cha Micharazo Time kutoka 98.4 Dodoma Fm Radio @wyse_tz amekanusha tetesi za kuwa @iambenpol amekuwa akijependelea katika suala la kuachia nyimbo kwani amekuwa akitoa nyimbo nyingi kuliko msanii wake, @wyse_tz amesema si kweli kama anabaniwa kwani vyote hivo vilisababishwa na yeye kuwa masomoni lakini kwasasa amesjipanga kuwafurahisha mashabiki.

Upande wa kuhusishwa kumtelekeza mpenzi alikuwa nae Dodoma WYSE amesema kwasasa anampenzi mpya ambaye ni mtu maarufu nchini na wamepanga kutoyaweka wazi mahusiano yao, kama mwanamke huyo ni msanii wa muziki, video queen au muigizaji wa filamu wyse1 hakuwa tayri kuelezea nakusema watu wake wa nyuma waliachana ka watu wengine wanavyoachama.

@wyse_tz Ameyataja mafanikio aliyoyapata baada yakurudia wimbo wa msanii @symplysimi wimbo wa joromi ni pamoja na kutafutwa na msanii huyo ambaye alimtaarifu kupenda sauti yake na tayari wameshaanza kuandaa wimbo ambao Wyse1 ataimba na msanii anaesimamiwa na SIMI.

SOUCE: MICHARAZO TIME 98.4 DODOMA FM RADIO
@benedict_ngelangela.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages