Chamwino Dodoma
Kata ya Iringa
Mvumi Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa
akiba ya chakula cha kutosha ili kukidhi mahitaji ya familia kwa wakazi wa Kata
hiyo.
Wakiongea na
kituo hiki baadhi ya wakazi wa kata hiyo akiwemo Bw Bi. Lucy Mathias pamoja na
Daniel Masanika wamesema hali hiyo inatokana
na kukosekana kwa mvua za kutosha hatua ambayo imechangia kwa kiasi
kikubwa uhaba wa chakula.
Aidha
wananchi hao wamesema kutokana na kujitokeza kwa hali hiyo imechangia kupanda
kwa bei za mazao ambapo kwa sasa wananchi hao wanalazimika kununua debe la
mahindi kwa kiasi cha shilingi elfu 22-25.
Diwani wa Kata
hiyo Bw. Robert Chikole Mwaliko amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza
sababu zilizo sababisha hali hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa mvua za kutosha
hatua ambayo imechangia mazao kunyauka na hivyo kila mwananchi anapaswa kutumia
vizuri akiba ya chakula kilichopo.
Wakati hayo
yakijili, mapema hapo jana Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu
Majaliwa akihutubia katika sherehe za Idd El Fitri Mkoani Kilimanjaro
alisisitiza wafanyabiashara kuacha kuuza mazao ya chakula nje ya nchi na badala
yake mazao hayo yauzwe katika Mikoa ambayo inakabiliwa na changamoto ya uhaba
wa chakula.