Siku moja
baada ya mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Bi. Christina Mdeme kuitisha mkutano na
wenyeviti wa serikali za mitaa juu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya baadhi
ya wenyeviti hao wameahidi kupambana vikali ili kutokomeza vitendo hivyo.

Akiongea na
kituo hiki Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Dodoma Bw.
Matwiga Kiatya amesema kwa kuzingatia agizo la mkuu wa Wilaya wenyeviti wote wa
serikali za mitaa katika manispaa ya dodoma wako tayari kupambana ili
kutokomeza matumzi ya dawa za kulevya.
Bw. Matwiga
amesema ili kutokomeza utumiaji na usambazaji wa dawa za hizo inapaswa kubaini
hasa vyanzo vya upatikanaji wake huku mtaa wa Chadulu ukionekana kuwa Mtaa
unaoongoza kushamili kwa matumizi ya dawa za kulevya.
Baadhi ya
wenyeviti wa Serikali za Mitaa akiwemo Bw. Mohamed Ramadhani kutoka mtaa wa
Chidachi pamoja na Bi. Helena Matonya kutoka mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji
wamekiri kuwepo kwa watu wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya katika
maeneo yao na kuahidi kuwa wako tayari kuhakikisha vitendo hivyo vinafikia
kikomo.
Utekelezaji
huo unaanza ikiwa ni agizo la mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini kutoa maelekezo
kwa wenyeviti wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Dodoma kusimamia zoezi
hilo huku mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Dodoma SSP Daniel Shilaha akitaja
baadhi ya Mitaa ambayo inaongoza kwa vitendo hivyo.
sanjari na hayo mwenyekiti wa wenyeviti mkoa wa Dodoma Bw Matwiga kupitia kipindi cha Dodoma live mkoani 98.4 Dodoma fm amesema watumiaji wanatakiwa kujitokeza wenyewe bila kutafutwa na polisi.
Na Pius Jayunga 98.4 dodoma fm radio.