Meneja wa timu ya BAOBAB QUEENS Matereka Junior kupitia mitandao ya kijamii ametoa taarifa hii kwa wapenzi wa soko mkoani Dodoma juu ya mechi ya kirafiki ya timu hiyo.
TAARIFA TOKA BAOBAB QUEENS.
Mwanadodomiya hii inakuhusu.... Mwakilishi pekee wa ligi kuu soka wanawake tz ambao ni baobab queens Jumapili hii itacheza mchezo wa awali kabla ya ngao ya hisani ligi ya mkoa do saa 8 mchana dhidi ya Pentagon Boys.
Mchezo ni mwendelezo wa kuiweka sawa kabla ya kucheza mchezo wa kwanza wa ligi na wageni wetu Kagera Queens Novemba mosi.
Njoo uione timu mwakilishi wa dom ligi kuu wanawake tz.
@BaobabQueens.