Timu ya CDA mkoani Dodoma ilisafiri na kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya MILAMBO FC ya mkoani humo katika mchezo wa ligi ya daraja LA pili.
Msemaji wa timu hiyo ya CDA amesema timu yao ilianza kuongoza kwakutangulia mbele kwa goli moja lakini kutokana na wachezaji wa mchezo huo kuonesha upendeleo kwa timu wenyeji iliwasadia timu ya MILAMBO kusawazisha goli na mchezo kumalizika kwa sare.
Timu hiyo ya CDA inatarajia kuanza safari ya kurudi mkoani dodoma siku ya kesho.
Na benedict ngelangela.