
Mgombea wa Urais wa CCM Dr John Pombe Magufuli leo amewapongeza wasanii @diamondplatnumz @ommydimpoz na @vanessamdee kwa ushindi wao waliopata katika tuzo za Afrimma zilizofanyika huko Marekani. Magufuli ambaye amekuwa akitembea na baadhi ya wasanii katika kampeni zake za uraisi amewaahidi kwamba hatowatupa baada ya kampeni.
