Ronaldo akishangilia bao lake la pili na Gareth Bale |
MAGOLI mawili yaliyotokana na mikwaju ya penati iliyowekwa kimiani na Cristiano Ronaldo usiku wa jana yalitosha kuipelekea Real Madrid hadi Fainali za Kombe la Mfalme wakiing'oa Atletico Madrid kwa mabao 5-0.
Katika mechi ya awali Real iliwaadhibu mahasimu wao hao wa jiji la Madrid kwa mabao 3-0 na hivyo ushindi wao wa jana umeifanya kutinga fainali kwa kishindo na kusubiri kukabiliana na mshindi kati ya Barcelona na .Real Sociadad
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kesho baada ya mechi ya kwanza Barcelona kushinda nyumbani mabao 2-0 na kunusua hatua hiyo ya fainali.
Ronaldo aliyekosekana katika pambano la Ligi Kuu ya Hispania wikiendi iliyopita kutokana na kutumia kadi nyekundu alitunga mikwaju hiyo katika dakika za saba na 16.