Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar,
ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala Mianzini jijini Dar es
Salaam, ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi wak
Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa
na shule ya awali ya Ali Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo jana saa
12.10 jioni kwenye eneo la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na
kiwiliwili
(hudugu)
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia
mauaji hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi
waliomuua ustadhi huyo.
Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.
"Ilidaiwa
kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa
kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili wake
kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.
Baada
ya mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na
kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo
hapo.
Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.
Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi