Kaa tayari kwa ajili ya wimbo huu mpya wa Snura Mushi. Unaojulikana kama Ushaharibu, Huu wimbo Unawazungumzia watu wenye tabia
yakuiangalia leo na kuidharau kesho, kwa mfano kuna watu Wamezungumziwa umo
ndani kuwa ''Uliuza nyumba kwa ugumu wa maisha,huna pakulala shida Umezizidisha,
Na haya ndio mashahiri ya wimbo huu wa ushaharibu....
Verse ya 1
Unatafuta kick na upo kwenye muziki, Ndio kwanza unahit
umetukana mashabiki
Ulikimbia wazazi ukayafanye mabaya, Tena ulimwaga radhi na
umepata miwaya
Ulitukana wakunga na wakati una mimba, Ulijiona mjanja kumbe wewe ndio mjinga
Umeombewa kulala umekojoa kitandani, Umetutia haibu kwenye
chumba cha jirani
Uliuza nyumba kwa ugumu wa maisha , Una pakulala shida
umezizidisha,
Kuto kujiamini umetapatapa, Umeliacha dume umelamba galasa.x
2
Chorus
Ndo basi tena ushaharibu,uuuhu
Kujifanya mjuaji ushahaaribuuuuhu
Umejitia ufundi ushaharibuuuuhu
Jipange upya ushaharibuuuuuuhu x 2
Vers ya 2
Unataka heshima kutoka kwa wako wana , Mbele ya watoto wako
matusi unatukana,
Baba yupo ICU mmeukata umeme, Tena mmeshaharibu wacheni mimi
niseme.
Nilipokuwa chini ulikuwa unitaki,leo hii niko juu unataka
urafiki.
Umechomwa sindano na umemeza vidonge, Ulivyo na dharau eti
umekunywa pombe.
Uliuza nyumba kwa ugumu wa maisha , Una pakulala shida
umezizidisha,
Kuto kujiamini umetapatapa, Umeliacha dume umelamba galasa.x
2
chorus
Ndo basi tena ushaharibu,uuuhu
Kujifanya mjuaji ushahaaribuuuu
Umejitia ufundi ushaharibuuuu
Jipange upya ushaharibuuuuh
x 2
Bridge
Ebu jaribu sasa kufikiria jambo usiharibu, Umeharibu sasa
limekushuka sura ina haibu.
Ebu chunga uchunge uchungweee usiharibu tena.
Hk chunga
uchungwe usiharibu tena,
We Snura chunga Uchungweeee.
Baby talha chungwa
uchungweeeee,
Na mapacha chungwa uchungweeee msiharibu tenaa.
Ebu chungwa
chunga uchungweee UsiharibuTenaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Kaa tayari kuupokea wimbo huu mzuri mwanzoni mwa mwenzi wa tatu.