BABY MADAHA: AMCHANA MBOVU SHILOLE, SOMA HAPA UJUE ALICHOMWAMBIA, YANI NI UTUMBO MTUPU
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Madaha’ amemchana staa mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumwambia ni mcheza muziki wa uswahilini (vigodoro). |
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Kauli hiyo ya msanii huyo anayetamba na Wimbo wa Summer Holyday,
ameitoa siku chache baada Shilole kutema cheche zake kuwa Madaha aache
kumfuatilia kwani amekuwa akiingia kwenye anga zake mara kwa mara.
Baby Joseph ‘Madaha’.
“Hivi huyu ana akili au matope, nimfuatefuate ana nini? Hebu aangalie
muziki wangu ninaopiga na wake. Yeye ni wa hapa hapa, mcheza vigodoro,”
alifunguka Madaha.