Mmoja wa wana
ndondi maarufu duniani na mkali katika kazi yake ametangaza siku ya
mwisho ya kuachana na kazi hiyo. Katika moja ya hafla iliyofanyika
wakati wa chakula cha jioni (January 17th)South Africa, Floy Mayweather ameripotiwa akisema kuwa “September 2015″ itakuwa ndio tarehe ya mpambano wake wa mwisho.
kwa bahati mbaya ripoti hiyo iliyotolewa na Associate Press inaweza ikapunguza nafasi ya kuwepo kwa mpambano kati yake na Manny
Pacquio ambao ulikuwa ukitarajiwa kufanyika kwa miaka mingi.
Ijumatano iliyopita (January 15th), Mayweather alisema kuwa Amir Khan
kutoka uingereza na Marcos Maidana kutoka Argentina inawezekana wakawa
ndio wagombea pinzanikatika pambano lake linalotarajiwa kufanyika tarehe
3 mwezi May, Las Vegas.
Floyd Mayweather ameanza kazi yake ndondi mwaka 1996 na ameshashinda michezo 45-0 na knokouts 26.