Shabaa limetoa makataa ya siku kumi na tano kwa wanaotoa huduma za internet kuzifunga
Wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na Al-Qaeda, wamesema kuwa wamepiga marufuku raia wanaoishi katika maeneo wanayodhibiti kutumia internet.Wapiganaji hao wametoa onyo kwa kampuni zote zinazotoa huduma ya internet siku 15 kufunga biashara zao.
"kampuni yoyote au mtu yeyote atakayepatikana akipuuza onyo hilo atajulikana kama mtu anayewafanyia kazi maaduzi zetu, na ataadhibiwa kulingana na sheria za ziisilamu,'' ilisema taarifa ya kundi hilo ambayo ilitumwa kwenye mitandao yake.
Wanamgambo
hao hutumia sheria kali za kiisilamu katika maeneo wanayotawala na
kuwakamata watu mara kwa mara kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Internet hutumiwa sana nchini Somalia, taifa ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, huku kundi hilo likionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa amani.
Internet hutumiwa sana nchini Somalia, taifa ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, huku kundi hilo likionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa amani.
Kundi
la Shebab zamani lilikuwa likitawala katika sehemu kubwa za Kusini mwa
Somalia na Kati, lakini likaondoa wapiganaji wake baada ya kushindwa na
wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaopambana nao.
Majeshi ya Afrika ikiwemo wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Kenya, tangu hapo wamedhibiti sehemu kadhaa kutoka kwa wapiganaji hao.
Majeshi ya Afrika ikiwemo wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Kenya, tangu hapo wamedhibiti sehemu kadhaa kutoka kwa wapiganaji hao.
Lakini
mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya maslahi ya
majeshi ya serikali na yale ya kigeni, yameondoa matumaini ya kunusuru
taifa hilo kutokana na vita vya miaka mingi.