Zitto
Kabwe leo ameendelea na ziara yake mkoani Kigoma ambapo kwa siku ya
leo alikuwa wilayani kasulu sehemu ambayo amepokelewa na wanachama wengi
wa Chadema pamoja na wananchi mbalimbali,Mapokezi yalianzia Kilombero kilometa 10 kutoka Kasulu Mjini.

Mapokezi
yalianzia ofisi ya Chadema jimbo la Kasulu Mjini ambapo Zitto Kabwe
alienda kusaini kabla ya kuendelea na taratibu zingine kisha alienda
kuongea na wazee wa Kasulu kwenye ukumbi wa chuo cha TTC,baadae
kuelekea moja kwa moja uwanja wa shule ya msingi Kijanamo sehemu
ulipofanyika mkutano.
Moja
ya vitu vilivyo make Headline leo kwenye mkutano huu ni kitendo cha
wazee wa Kasulu kumsimika rasmi u-chifu Zitto Kabwe kutoka jina
analolitumia la Zitto Kabwe mpaka kuitwa Wami Bhiyagwa jina lenye sifa
ya mtu anayetenda matendo mazuri na kukubalika na watu wengi.
‘Sina
namna ya kueleza furaha niliyonayo kwa mapokezi makubwa mliyonipa
kasulu,Hii ni salamu tosha wajue na mimi nina kwetu,toka nimefika
kilombero mpaka naingia kasulu mjini nimeona nyuso za watu,wazee na kina
mama zikiniombea kila la kheri yanayonikuta sasa yapite ili tuendelea
kutetea maslahi ya mkoa wetu na nchi yetu na kwa uwezo wa mungu
yatapita’.
‘Kwangu
mimi mambo yote nayaona kama changamoto ya Maisha,maana yake hata
Dhahabu ili iwezekuwa Dhahabu lazima ipite kwenye moto,kwa hiyo haya
yanayotokea yananipa nguvu zaidi na anayefikiri kama yananinyong’onyesha
asahau,kwa sababu watu wa Kigoma wana sema nguvu ya Mamba kumai,nguvu
ya mwanasisasa ni watu na watu ndo nyie’







Post Top Ad
Responsive Ads Here
Sunday, December 22, 2013

TAZAMA JINSI ZITTO KABWE ALIVYOSIMIKWA UCHIFU WILAYANI KASULU KIGOMA.
Tags
# NEWS
Share This
About inngelangelanews.blogspot.com
NEWS
Labels:
NEWS
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.