
kuimba ni kutokana na kumkubali sana mwanadada ''Lady Jay Dee'' kwa style ya uimbaji pamoja na kujiheshimu, ''Neecia'' hakuishia hapo alitiririka kwamba moja kati ya vitu vinavyo sababisha amkubali Jide ni kudumu kwenye game kwa muda mrefu bila kutetereka. Mazungumzo na mwandishi yalikuwa hivi-
Mwandishi: Una umri wa miaka mingapi na una vipaji vingapi?
Neeccia: Mbali na Umodo pia naimba mziki...
Mwandishi: Umeanza muziki lini na mpaka sasa una singo ngapi?
Neeccia: Nimeanza muziki mwaka 2005
nikiwa na umri wa miaka 14 kipindi hicho niko kidato cha 1 kiukweli
muziki ulinigombanisha sana na wazazi wangu ila nikakomaa mpaka leo nna
singo nyingi ila natarajia kuachia mbili kwanza.
Mwandishi: Enhee.. Hebu niambie upande wa umodo ulivutiwa na nani hasa mpaka ukajikuta ndani ya ishu hiyo ya ?
Neeccia: Mimi tangu enzi hizo
nilivutiwa sana na mwanadada Miriam Odemba. Hata napowaza kushiriki
katika mambo haya huwa natamani nifike alipofika.
Mwandishi: Mpaka hapo nadhani wasomaji wangu watakuelewa nakupa nafasi uwaage wasomaji wangu kwa chochote.
Neeccia: Kwa sasa
nawaomba wadau wa website ya www.masainyotambofu.com wanipigie kura
kwenye mchuano wa Miss Beer Worldwide Model Contest kunipigia kura
bonyeza link hii hapa chini--http://www.missbeer.org/contestant/8489