Jaji Sekieti Kihio |
JAJI mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa Sekieti Kihio amesema kuwa wapo baadhi ya watu wenye mawazo potofu kuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wa serikali wapo juu ya sheria hivyo hivyo hawapaswi kuzingatia sheria za nchi jambo ambalo halina ukweli na kuwa kila mmoja wetu akiwemo Rais anapaswa kuzingatia sheria mbali mbali na kuheshimu maamuzi ya mahakama.
"Msemo kuwa mfalme hawezi kutenda kosa hauna nafasi katika sheria zetu hata kama neno Rais litasimama badala ya neno mfalme kila mtu na kila Taasisi au shirika katika nchi hii wote wanatakiwa kuheshimu misingi ya ukuu wa sheria"
Jaji Kihio alitoa kauli hiyo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini sherehe zilizofanyika katika viwanja vya mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa na kuwa suala la utawala wa sheria ama upatikanaji wa haki inataka kuwa vyombo vinavyotoa haki vifikike kwa wale ambao haki zao zimevunjwa wakiwemo raia ambao haki zao zimeathiriwa na vitendo vya watendaji mbali mbali wa serikalini pia waweze kudai haki zao katika vyombo vinavyotoa haki kwa uhuru bila woga au upembeleo.
"Sina Shaka kuwaeleza kuwa falsafa ya mgawanyo wa madaraka ya dola ina mahusiano ya karibu na dhana ya utawala wa sheria ...serikali ambayo imehodhi mamalaka yote ya dola yaani bunge ,utawala na mahakama ambayo ina nia ya mabavu itapitisha sheria yoyote inayotaka kama alivyowahi kusema jaji mkuu wa Uganda jaji Benjamini J. Odoki katika mada yake Uimarishaji wa utawala wa sheria huko Nairobi April 6 mwaka 2005 katika moja kati ya kongamano kuwa serikali inayohodhi madaraka yote ya dola itazitumia sheria ilizozipitisha kinyama bila kujali haki na uhuru wa wananchi na kama mmoja wa wananchi anazipinga sheria hizo serikali hiyo itamhukumu bila kujali misingi ya utawala wa sheria"
Jaji Kihio alisema kuwa bila utawala wa sheria nchini migogoro ,mivutano ,ushindani wa kisiasa na kibiashara na hata tamaduni vitaendelea kushamiri na vitapata suluhu si kwa njia ya majadiliano bali kwa mabavu ,vitisho ,kutiana vilema ama kuuwawa ambapo matokeo yake ni amani kutoweka hivyo ili Taifa liendelee kuwa na amani ni vema viongozi wa umma kuepuka kuingilia uhuru wa mahakama katika utendaji kazi wake.
Alisema kuwa bila kuwepo kwa utawala wa sheria nchi inaweza kujikuta ikiingia katika machafuko yasiyokuwa ya lazima kwa vile kila mtu hasa viongozi watakuwa na uhuru wa kutoa maagizo yoyote ya kiimla ili kusudi tu waweze kutekeleza matakwa yao.
Hata hivyo alisema kuwa kesi nyingi zinashindwa kusikilizwa na kumalizika kwa wakati kutokana na kiasi kidogo cha fedha kinachoingizwa kwenye mfuko maalum wa mahakama na matokeo yake mahakama inashindwa kutoa haki kwa washtakiwa kwa wakati na hivyo dhana ya utawala wa sheria kutia shaka katika akili za wananchi.
Alisema kuwa mfano kesi za makosa ya jinai zinachukua muda mrefu kwa sababu ya mashahidi hawaitwi kutokana na fedha kwa ajili ya kuwalipa mashahidi hao hazipo na hivyo haki zinacheleweshwa na kupelekea magereza mengi kufurika mahabusu .
Kwa upande wake mwanasheria mkuu wa serikali kanda ya Iringa Limail Manjoti mbali ya kuipongeza tume ya haki za binadamu na utawala bora kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa katiba ya sheria za nchi bado alikemea tabia ya baadjhi ya vyombo vya habari na wanasiasa kuingilia uhuru wa mahakama katika kesi ambazo bado kutolewa hukumu mafano kesi ya Dowans na TANESCO kuwa kwa kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Kwani alisema kuwa kufanya hivyo kunatoa taswira potofu kwa wananchi hasa pale maamuzi yatakapotolewa tofauti na matarajio ya wengi na kuwa kitendo cha kujadili masuala yaliyopo mahakamani ni kuingilia uhu
HABARI NA FRANCIS GODWINI