Katika kuadhimisha wiki la unywaji wa maziwa ambalo limehitishwa ijumaa ya tarehe 1 june 2018 kampuni ya uzalishaji na uuzaji wa maziwa nchini ASAS DIARIES Iliweza kugawa maziwa bure kwa baadhi ya Shule za msingi ambazo zinapatinakana katika jiji la Dodoma.
Takribani shule Tano zilifikiwa kwakutembelewa na kampuni hiyo, Na moja ya shule ambayo ilibahatika ni pamoja na Shule ya Msingi Nkuhungu ambayo inaidadi ya wanafunzi zaidi ya elfu tatu (3000+) na takribani ya wanafunzi wote waliofika siku hiyo walipata pakiti moja ya maziwa ya ASAS FRESH.
TAZAMA PICHA.