Wakazi Mkoani Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari
dhidi ya kundi la matapeli lililoibuka na kujitambulisha kwa kutumia simu za
mkononi kuwa ni watumishi wa manispaa ya Dodoma huku wakiwatapeli wananchi fedha
kwa madai kuwa wanatakiwa kulipia kodi za viwanja na majengo kwa njia ya simu.
Taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari na afisa habari na uhusiano Manispaa ya Dodoma Bw.
Ramadhani Juma inasema kuwa matapeli hao wamekuwa wakitumia vyeo mbalimbali na
kutaja gharama ya kodi hizo kuwa ni shilingi elfu 20 hadi elfu 25 kwa kodi za
viwanja na majengo
Aidha
matapeli hao wamekuwa wakiwataka watu kutuma sehemu ya fedha hizo kwa njia ya
simu na kiasi kinachobaki mhusika akiwasilishe katika ofisi za kata husika kitendo ambacho huwenda kikachafua sifa na uhusiano
mzuri baina ya wananchi na watumishi hususani watendaji wa kata na halmashauri
Katika hatua
nyingine uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma umeahidi kuendelea kufuatilia
kwa karibu wahusika wa vitendo hivyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa
kwa mtu yeyote atakaebainika kuhusika katika vitendo hivyo.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma Fm
Radio