
Akizungumza na kipindi cha micharazo time cha 98.4 dodoma fm radio Onesix amesema amekuwa akisumbuliwa na homa ambayo inapelekea kuushiwa nguvu nakushindwa kufanya kazi ya aina yoyote huku tumbo na kichwa vikiuma kwa muda mrefu hali iliyopelekea madaktari kumwambia apumzike.
Hali hiyo imepelekea msanii huyo kusitisha shughuli zake za muziki kwasasa hadi pale atakapo pata nafuu na nguvu yakuendelea na kazi hiyo pamoja kupiga show ambazo kwakipindi hiki imekuwa nguvu kuzipokea kabisa.
amesema pia kwasasa alikua mbioni kuachia video yake mpya lakini imeshindikina kutokana na kuumwa kwani alitarajia kuachia video na audio mwezi wa saba.