![]() |
| nyama ya nguruwe |
kwaupande mwingine Wafugaji wa nguruwe
wametakiwa kufuga ufugaji wa ndani sambamba na
kuacha kulisha nguruwe mabaki ya
vyakula vya binadamu na mizoga ili kuweza kuepuka ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Daktari wa mifugo mkoa
wa Dodoma Godluck Ndaweka amewatahadharisha wafugaji wa nguruwe kuwa ugonjwa wa
homa ya nguruwe hauna tiba hivyo jamii inapaswa kuchukua tahadhari kwa
kuzingatia usafi katika mabanda ya nguruwe na kuepuka kuwalisha mabaki ya
vyakula vya wanadamu.
Aidha amesema kuwa
unaweza kumgundua nguruwe mwenye homa ya nguruwe kupitia dalili mbalimbali
ikiwamo nguruwe kushindwa kula
,kutetemeka sambamba na kuwa na mabaka mekundu sehemu za miguu na mgongoni pia
vifo vyao huwa vya ghafla.
Dr Ndaweka amesema
pamoja na kwamba ugonjwa wa homa ya nguruwe hauwezi kumpata mwanadamu lakini
madaktari wa mifugo hawashauri kutumia kitoweo hicho kwa nguruwe ambao
wanaugonjwa huo.
