(AUDIO)MITAA INAYOONGOZA KWA MATUMIZI YA MADAWA YAKULEVYA MKOANI DODOMA YATAJWA CHADURU INAONGOZA, MITAA MINGINE NI...... - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, February 17, 2017

(AUDIO)MITAA INAYOONGOZA KWA MATUMIZI YA MADAWA YAKULEVYA MKOANI DODOMA YATAJWA CHADURU INAONGOZA, MITAA MINGINE NI......

  Upambanaji wa madawa yakulevya mkoani Dodoma wapamba moto huku wenyeviti wa mitaa wakitakiwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kutokomeza madawa yakulevya mitaani. ipo baadhi ya mitaa iliyotajwa kuwa inaongoza kwa vijana wengi kujikita kwenye matumizi ya madawa yakulevya.
 Image result for MADAWA YAKULEVYA
Mitaa hiyo nayo ni CHADURU ambayo imeonekana ndiko kwenye tatizo kubwa zaidi ikifutia na kata ya MAJENGO, kata ya MAILI MBILI, kata ya BAHI ROAD pamoja na KIZOTA huko ndiko ambako imeonekana kuwa ni tatizo sugu na mitaa hiyo ilitajwa na mkuu wa jeshi lapolisi mkoa wa Dodoma SSP Daniel Shilaha.

Akiongea na kituo hiki Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Dodoma Bw. Matwiga Kiatya amesema kwa kuzingatia agizo la mkuu wa Wilaya wenyeviti wote wa serikali za mitaa katika manispaa ya dodoma wako tayari kupambana ili kutokomeza matumzi ya dawa za kulevya.
Bw. Matwiga amesema ili kutokomeza utumiaji na usambazaji wa dawa za hizo inapaswa kubaini hasa vyanzo vya upatikanaji wake huku mtaa wa Chadulu ukionekana kuwa Mtaa unaoongoza kushamili kwa matumizi ya dawa za kulevya.
Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa akiwemo Bw. Mohamed Ramadhani kutoka mtaa wa Chidachi pamoja na Bi. Helena Matonya kutoka mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji wamekiri kuwepo kwa watu wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao na kuahidi kuwa wako tayari kuhakikisha vitendo hivyo vinafikia kikomo.
Utekelezaji huo unaanza ikiwa ni agizo la mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini kutoa maelekezo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Dodoma kusimamia zoezi hilo huku mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Dodoma SSP Daniel Shilaha akitaja baadhi ya Mitaa ambayo inaongoza kwa vitendo hivyo.

sanjari na hayo mwenyekiti wa wenyeviti mkoa wa Dodoma Bw Matwiga kupitia kipindi cha Dodoma live mkoani 98.4 Dodoma fm amesema watumiaji wanatakiwa kujitokeza wenyewe bila kutafutwa na polisi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages