LIGI YA BASKET BALL YANOGA DODOMA, MIHUJI YAIKUNG'UTA MAKOLE - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, February 19, 2017

LIGI YA BASKET BALL YANOGA DODOMA, MIHUJI YAIKUNG'UTA MAKOLE

leo ndani ya mkoa wa dodoma kumeanza ligi ya mpira wa kikapu ulio zikutanisha timu mbili ambayo ni makole pamoja na mihuji na timu inayo wakilisha Mihuji kuibuka mshindi wa vikapu 61 kwa 56 Dhidi ya makole.

ligi hiyo inayokutanisha mitaa mbalimbali ndani ya manispaa ya Dodoma ambayo imelenga kuibua vipaji ambavyo vimejificha pamoja na kuhamisisha ukuzaji wa mchezo huo ndani ya mkoa huu wa dodoma.

timu ya mihuji
mchezo kati ya MIHUJI na MAKOLE ulianza kwa kila mmoja kuonesha uchu wa kutaka kuibuka ushindi lakini kila kwenye ushindani ni lazima mmoja ashinde na mwingine ashindwe ndipo MIHUJI ilivyo jitutumua kwa kuongoza katika round zote nne.
timu ya makole
Katika mchezo huo round ya kwanza ilianza kwa MIHUJI kuongoza kwa jumla ya vikapu 20 huku MAKOLE wakiambulia vikapu 10.
round ya 2.
MIHUJI vikapu 35 MAKOLE 28

ROUND 3
MIHUJI vikapu 41 MAKOLE 38.

ROUND 4.
MIHUJI vikapu 61 MAKOLE 56.

Mpaka mchezo unamalizika MIHUJI imeibuka na ushindi wa vikapu 61 kwa 56 dhidi ya MAKOLE.


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages