Msanii wa muziki kutoka Dodoma One Six amesema angepata nafasi ya kushiriki kwenye wimbo mpya wa msanii STAMINA ambao kamshirikisha MR BLUE angefanya makubwa kuliko haya yaliyofanyika sasa.
 |
onesix |
Akizungumza kupitia kipindi cha Micharazo time toka 98.4 Dodoma Fm radio na Benedict Ngelangela, ONESIX amesema amefurahishwa sana na kitendo cha STAMINA kurudia wimbo wa msanii mwenzake BAGHDAD ambao yeye mwenyewe alishiriki kwenye uimbaji wa chorus ya awali.
ONESIX pia amesifia kile kilichofanywa na Mr Blue kwani amepiga bonge moja la Chorus ambayo si rahisi kufanywa na mtu yoyote, ila ameongeza kwa kusema endapo angepewa nafasi yakuifanya iyo Chorus angefanya poa zaidi kuliko hata ya kwanza ambayo alifanya na Bagdhad.
ONESIX kwasasa anatamba na kibao chake cha Mama Dont cry ambayo anatarajia kuitoa hivi karibuni.