Msanii wa muziki kutoka Dodoma Brezy amesema hana tatizo ba msanii mwenzake wa muziki ambae pia ni mrayarishaji wa muziki.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Micharazo Time kutoka Dodoma FM radio Benedict Ngelangela alipoulizwa kama anatatizo na msanii huyo Brezy amesema huwa anasikia tu izo tetesi lakini hajui kama aliwahi kugombana nae ila huwa anasikia tu kuwa yeye na Jaco Beat hawaelewani.
Alipoulizwa kama anaweza kufanya kazi na msanii huyo Brezy amesema kwasasa hajafikiria jambo kama hilo kwani malengo ni kufikisha muziki wake mbali, ila pia alisisitiza kuwa hana tatizo na Jaco ila anahisi jaco ndo anatatizo na yeye.
Kwasasa Brezy anawimbo wake mpya unaitwa Zakora.