MAKALA:WASANII WA DODOMA WANAVYOKULA UGALI KWA PICHA YA SAMAKI. - MOE KALI - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, September 19, 2016

MAKALA:WASANII WA DODOMA WANAVYOKULA UGALI KWA PICHA YA SAMAKI. - MOE KALI

 
WASANII WA MUZIKI NA FILAMU. Umewahi sikia huu msemo? Maana yake unaifahamu? Basi ngoja Leo nikujuze maana yake vizuri. Miaka michache ya nyuma kuna Tamthilia moja hivi iliitwa jumba la dhahabu,hii ilikuwa n moja ya tamthilia nzuri saaana na moja ya tamthilia zilizofanya mapinduzi kwa miaka kadhaa baada ya Tamthilia Pendwa za Kaole na Mambo hayo kupotea kwenye ramani. Basi bana,yule Tues akaja Dodoma na kufanya usaili wa wasanii wa maigizo ili awape fursa. Wasanii wakawa na vipaji vyao wakaenda kuonesha manjonjo yao. Unajua kilichowakuta,sidhani hata kama Morogoro walifika. Wakarudi na vipaji vyao wakakaa tena Mambo Poa na Mapinduzi. 

UNAWAKUMBUKA JB,AUNT EZEKIEL walikuja wakati fulan hivi wa Fiesta kutafuta vipaji,usaili ulikuwa pale Club Laazizi. Watu walienda bana na Ugali wao wakitegemea watakuta samaki aliyekaangwa vyema,kachumbali na pilipili. Ila waliambulia kula ugali wao kwa picha ya samaki. Unajua kilichowakuta? Waliambiwa "WASANII WA DODOMA MNAJUA 

 SANA,MNAWEZA FANYA MAPINDUZI".Wakaridhika wakarudi Mapinduzi na Mambo poa kufanya Mazoez wajiandae na Mapinduzi. Hakuna kujitambua,hivi wewe msanii NA akili zako unaenda panga folen JB na Aunt wajufanyie usaili una akili timamu kweli? Wale n Special Appearance sio wakutafuta viapaji. Wana walimu wao,hao ndio watakupa sumu ya hao kufika hapo. MFANO MDOGO.Unaangalia BSS? umewahi ona majaji wa pale? Sio wasanii wa music ni walimu wa music. Angalia hata Tusker P.F.Wewe unaenda kupiga nao Picha na kutusumbua mitandaoni tu. Unaenda NA ugali wenzako wanakupa picha ya samaki unakula ugali unajiona wewe unajua. 

Unaikumbuka Super Nyota? Hapa alitoka msanii mmoja anaitwa Jaco Beats. Eti yuko wapi Leo? Alienda mpaka kule kwao,na kuingia kabisa katika ofisi zao akala bata kwa kupiga picha nao akarudi Dodoma. Unadhani ukimuona kamzidi nn One Six,Breezy,Mchungaji Zayumba. Wako wote pale mitaa ya Chako ni Chako kwa Kimambo wanatengeneza mziki tu. 

Unakumbuka Tuzo za NYAMBAGO Season One? hizi zilikuwa na wagen toka Dar,alikuwepo mtayarishaji bora kabisa wa mziki BoB Junior. Alishinda msanii bora wa kiume One Six,Bob Junior akamuahidi kumrekodia ngoma yake bure..ahahahhahaha hapa siongei sana,mtafute Sulesh (Muandaaji WA Tuzo) na One Six halafu mpigie simu Bob Junior atakwambia kiliendelea nini. JOHN LISTER moja ya waongozaji wazuri wa Film,walikuwepo katika Tuzo za Season 1. Alimuahidi Mch.Zayumba kumtengenezea Kichupa kikali,hapa sihitaji maswali,labda wanajiandaa kwenda South Africa kupiga kichupa. 

Fiesta Imooooo......eeee ilikuwemo kweli,WASANII walifika kama kawaida. Wakapanda jukwaani. Wakaimba,wakapiga PICHA na wasanii wakaweka mitandaoni kuonesha wako nao pamoja. Wakaimba kurasa za Tovuti za DODOMA zikaandika "WASANII WA DODOMA WASHAMBULIA JUKWAA LA FIESTA". Hapo ndio utaona tofauti ya kuimba mwanzo au mwisho WA show. Mwanzo unaweza kuwa unatest Mic na watu ndio wanazidi kuingia. Lakini mwisho unaweza kuimba kama enzi zile tunaita fungulia Dog. Yaani wakati wanaanza kukusanya vitu vyao ndio unaimba. Unapiga picha unatusumbua mitandaoni tu.
MWISHO. 

Hii sio Dodoma Kwanza tunayoitaka,tunataka Dodoma Kwanza itakayofunguka NA kuwa wawazi bila kuogopa mtu. Huu sio muda wa siasa. Tunataka tengeneza soko la ndani kwanza,tusiwaze Clouds atusaidie kutengeneza wasanii wetu. Yeye mwenyewe anawaza soko lake la ndani. Ana THT WASANII wako folen wanamtazama yeye,wewe Dodoma unakaa vikao kujadili atakusaidiaje. Tuna Redio zaidi ya 10 Dodoma sasa,hizi Radio zinasikilizwa na watu na watangazaji wanajua sana kupanga vipindi tunashindwa nn kuziremote NA Dodoma Kwanza kupiga mziki wetu? Usiseme hawawezi. Ukienda Dar kuna Radio inaitwa EFM,hii Radio ilikuja na style yake mpya,nina imani bila EFM usingemfahama Man4ngo. Iliutengeneza mziki wa Singeli kuwa mpyaaa.. Leo kila mtu anauimba,Man4ngo sio level za SUPER NYOTA Jaco beats. Tutengeneze soko la ndani na linawezekana sana tu. Ila n kupata watu kwenye njaa NA WASANII sio hao wenye kazi zao tayari,mwisho WA mwez wanapokea mshahara huku wasanii hawajui hata mchana atakula nini.


Film zinaenda kwa taabu sana,kila mtu anamuwaza Steps tu,Steps ni soko la ndani la Dar,sisi tutengeneze la kwetu. Hujiulizi kwann WASANII wanakimbilia Dar? Wanafata soko la ndani kule. Sisi tunafeli nn? Tunazidiwa ubunifu na Mpwapwa Entertainment. 

Tutaendelea kutembea na vipaji vyetu kama Ugali tu. Tukifika kwa wenyewe wanatupa picha ya SAMAKI tunakula UGALI wetu halafu tunarudi tulikotoka.
"DODOMA KWANZA"

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages