LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU) SEHEMU YA 6 & 7 - NGELANGELA NEWS

Post Top Ad

Tuesday, August 30, 2016

demo-image

LOVE IS PATIENCE (MAPENZI NI UVUMILIVU) SEHEMU YA 6 & 7

Responsive Ads Here

Love is patience
Mtunzi; lulu hamza
Sehemu ya sita
 ?ui=2&ik=0c85e109a2&view=fimg&th=156972b055ed14a4&attid=0
Ilipoishia
Joseph akiwa katoka kumuelezea mama yake kuwa anaitaji kuoa ila majibu ya mama yake yalimshitua kidogo.
Endelea
“Mbona unanishanga hivyo mwanangu?” “Hapana mama nashanga nimeongea habari za kuoa ujanisikiliza unamtaja Joyce siielewi unachoongea”. Mama joseph akacheka kwa kejeri “khaa!! Leo umenifurahisha uelewi nini sasa mwanangu, namaanisha mkeo mtarajiwa Joyce” “mwanamke nayetaka mimi kumuoa sio huyo Joyce, na sijui umepata wapi hizo habari za Joyce”. Mama yake akaacha kazi aliyokuwa anaifanya muda wote na kumgeukia mtoto wake kama mtu aliyeshanga sana “mbona unataka kunichanganya wewe mtoto, embu nieleze vizuri binti gani unataka kutuletea hapa nyumbani tofauti na Joyce?”.
“Kwani imekuwaje ufikirie kuwa namleta Joyce hapa ndani kwanini nimlete yule mtoto hapa” “haya mtaje huyo mwanamke” “ni Prisca mchumba wangu” “Prisca!! Yupi? Huyu mfanyakazi wa baba yako?” “Ndio huyo huyo”. “Nani kakwambia utembe na yule binti? Binti muhuni ofisi nzima inajua wewe ndio unataka kumletea baba yako” “uhuni wake nini mama, mbona mimi sijausikia siku zote?” “Embu tulia kwanza tutaongea baadae, nenda kapumzike”. Joseph aliingia ndani akiwa na mawazo mengi “hivi mama anamaanisha anachoongea kweli nimuoe mtoto wa rafiki yao ila kwanini nimuoe joyce? Ngoja nimsubiri hiyo baadae”.
Jioni Wakiwa mezani wanakula, Joseph alijikuta kapaliwa na chakula baada ya kusikia haya maneno ya mama yake. “mtoto wako anataka kumuoa Prisca eti” baada ya hayo maneno wote wakawa kimya Joseph akamtolea mama yake macho, Josephine naye akabaki anasikiliza baba yake anajibu nini. “Prisca? Kwanini unataka kumuoa Prisca na kwanini unataka kuoa sahivi?” Joseph alivuta pumzi kwanza “mimi nadhani niko tayari kuoa baba na ndio mwanamke naye mpenda” “upo tayari? Kwa kipi hasa upo tayari” “niko kazini baba nitajijenga na mke wangu nadhani”.
Baba yake alimsogeza sahani yake ya chakula kwa hasira sana “acha ujinga wewe mtoto wa kiume sijui kwanini unaakili ya kike hivyo..” Joseph alimuangalia baba yake jicho la hasira ila akabaki kimya. “Hakuna ndoa itakayo fungwa ukiwa katika hali hii, na kama utaitaji ndoa binti wa kumuoa ni Joyce pekee yake sio hao wamalaya unaowaokota huko”  “lakini baba mambo ya kuchaguliana mke ni ya zamani” Josephine aliongea kwa hisia. “Embu kelele na wewe baba yako anaongea na kaka yako kwanini wewe uingilie” Joseph aliinuka na kuelekea chumbani kwake maana alikuwa ameshapata hasira na hakutaka kuwajibu wazazi wake kitu.
Asubuhi kama kawaida ya familia nzima kila mtu alijianda kwenda kazini, kasoro Josephine aliyekuwa yupo rikizo ya chuo. Joseph aliingia kwenye ofisi ya baba yake akiwa mpole sana alipita ofisi ya Prisca kabla ajaelekea kwenye kitengo chake “hey za Asubui mpenzi?”. “safi Prisca umeamkaje?” “Salama sijui wewe?” “Niko salama, sasa baadae kidogo nitakupitia kwenye chai” “sawa kazi njema”. Joseph aliingia ofisini kwake ilikuwa mida ya saa mbili asubuhi alishindwa kabisa kufanya kazi aliwafikiria wazazi wake akakosa majibu kabisa. Ghafra aliingia Jimson rafiki kipenzi wa Joseph “oi Joseph kuna nini kwani?” “kivipi?” “Kwanini Prisca kafukuzwa kazi kwa utaratibu ule alafu umekaa huku ndani, kwanini umesaini barua ya Prisca kufukuzwa”. Joseph alibaki anamshanga rafiki yake asijue kinachoendelea aliinuka haraka na kutoka nje alikuta kila mtu anasikitika kwanini Prisca afukuzwe na kachangia mambo makubwa sana kwenye kampuni.
Joseph aliingia moja kwa moja ofisini kwa baba yake, alikuwa ameshikwa na hasira ya hali ya juu “baba kwanini umemfukuza Prisca kazini?” “Unaniuliza ilo swali wewe kama nani kwenye kampuni yangu?”
Usikose itapoendelea
 ........................................................................................................


LOVE IS PATIENCE
SEHEMU YA SABA
MTUNZI; LULU HAMZA 
 0656994884
 ?ui=2&ik=0c85e109a2&view=fimg&th=156972b055ed14a4&attid=0
Ilipoishia
Prisca akiwa kafukuzwa kazini, Joseph aliingia ofisini kwa baba yake kumuuliza kwanini kufanya vile ila alipokea jibu moja la nguvu
Endelea
“Lakini baba mimi sidhani kama kulikuwa na haja ya kumfukuza mfanyakazi wako kazini, mtu ambaye ni mtendaji mzuri tungeyaongea tu yaishe” “wafanyakazi wapo wengi sana mwanangu, tutapata mwingine, siwezi kukaa na wafanyakazi wanao endekeza mapenzi kazini na wakubwa wao”. “Basi nifukuze mimi mrudishe yeye” “hapa harudi tena na ukiendelea kuwa naye nitamfata mpaka kwao, angalia maisha yako Joyce ni mtoto wa tajiri na wanakampuni Zaidi ya nne hapa nchini naitaji umuoe ..” “Sasa kampuni zao na mimi kumuoa vinaendana nini hapa baba?” “Yule ni mtoto wa kipekee na zile mali zote ni zake kwa hiyo ni lazima umuoe” “mnanichanganya”.
Joseph alitoka nje alichukua gari lake mpaka nyumbani kwa kina Prisca alimkuta Prisca amekaa tu nje ya geti lao. “Hey Prisca, mbona upo nje?” “Nafikiria cha kumueleza mama kwanini nimewai hivi kutoka kazini” “njoo kwenye gari tunaitaji kuongea” “kuongea nini Joseph, umesaini kabisa barua yangu niondolewe kazini nimefanya kosa gani? Na ni fedha gani zilizopotea?”. “sijasaini hiyo barua na ni baba ndio kufanya hivyo sababu jana nimewaambia nataka nikuoe, naomba twende sehemu tukaonge vizuri” Prisca alivuta pumzi kisha aliinuka na kupanda gari la Joseph. “Sawa twende” “asante kwa kukubali” Joseph aliondoka gari kwa mwendo mkali kidogo Waliingia kwenye hoteli iliyotulia kidogo joseph alimuelezea Prisca wazazi wake wamechukia yeye kuoa. Ila hakumtaja kabisa Joyce “na sababu nimekata kusimamisha ndoa yangu na yako na wao wakasema watakutoa kazini, ila sikudhani kama wanamaanisha walichoongea” “itakuwaje sasa?” “nitatafuta sehemu uendelee na kazi nikiendelea kuongea na wazazi wangu taratibu, wanaamini bado sijajipanga kuoa” “sawa basi”. “Rudi nyumbani kesho Asubui nitakupitia basi” “sawa Joseph” Prisca alirudi nyumbani, Joseph alizungukia ofisi za marafiki zake siku hiyo nzima.
Jioni aliingia nyumbani na kumkuta baba yake amekaa sebureni na Josephine, alisalimia akataka kwenda ndani ila baba yake alimuita. “naam baba” alirudi sebureni kumsikiliza baba yake anasema nini “kwanini haukuwepo kazini siku nzima na ulijua kuna kikao cha msingi?” “Samahani boss nilipita matatizo kidogo ya kifamilia na niliacha taarifa kwa Jimson”. Baba yake akawa kimya kidogo wote wakawa wanaangaliana “hayo mambo gani ya kifamilia ambayo mimi siyajui na sisi ndio familia yako” “mambo ya familia yangu mimi, sio ya hapa”. “usinijibu hivyo wewe mtoto, yaani unapoteza muda kwa kufanya mambo ya kipuuzi unaakili kweli wewe?” “Kwanini lakini mnanifanyia hivi lakini? Kwani kumpenda Prisca kuna tatizo gani?”. Mama yake Joseph alipita pembeni ya Joseph na kukaa kwenye kochi “hivi Joseph mwanangu unashida gani wewe? Kwanza yule binti ni mkubwa kwako miaka miwili kakuzidi. Hivi ni kweli unakosa watu wa umri wako au chini ya hapo”.
“Moyo wangu ndio umempenda yeye, sidhani kama umri ndio tatizo kubwa kiasi hicho hapa. Na sioni umuhimu wa kuliongelea hili” Joseph aliingia ndani kwa hasira akifunga mlango wake. Aliwaza sana nini afanye ila hakupata jibu “hapa ni bora nianze kutafuta kazi pia maana baba yangu hatabiriki”. Joseph alijilaza kitandani usingizi ukamchukua
Itaendelea . usikose kujua nini kitampata Joseph na Prisca

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *