
Ainea amesema alifanya kazi na producer huyo mwaka 2015 mwezi wa pili ambao alimuachia kimambo aendelee kuufanyia mixing kwani hakuwa na haraka ya kuuachia wimbo huo lakini amestushwa kuoona wimbo huo ukiwa umeenea kwenye Blogs mbalimbali.
Ainea ameongeza kwa kusema wimbo ambao umevuja ndio wimbo ambao alikuwa anategemea kuutoa hivi karibuni lakini ameumia zaidi kwani hali hiyo imesababisha kupoteza muelekeo wa kuendelea kupromote wimbo huo.
Alipo ulizwa kuwa ni kwanini ameamua kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii, Ainea amejibu sababu yakufanya hivyo ni kutokana na Producer huyo kutopokea simu zake kila akimpigia simu na anashindwa kuchukua hatua zozote kwasababu producer huyo hana studio maalumu.
Mtangazaji wa kipindi cha Micharazo pia alimtafuta producer wa wimbo huo ili kujia ni kwanini wimbo huo umeweza kuwafikia watu bila idhini ya msanii husika, Kimambo amesema hata yeye hafahamu ni nini kimetokea kwani aliibiwa simu mwaka jana akiwepo nchini Kenya(mombasa) na simu hiyo ilikuwa imejaa nyimbo za wasanii mbalimbali kwahiyo anahisi aliye ichukua simu hiyo ndiye alie vujisha wimbo huo.
![]() |
producer kimambo |
akijibu ni kwanini ahapokei simu za Ainea, kimambo amesema hutumia muda mwingi kulala kwani hukesha usiku mzima kufanya kazi zake za kimuziki.