Familia ya Sadalla mkoani dodoma pamoja na memba wa kundi la Wazawa unit siku ya jana wamepata pigo la kuondolewa na kijana wao aliyekuwa anafahamika kwa jina la Gifted Sadala wa mvumi makulu.
kupitia vipindi mbalimbali vya radio tofauti tofauti mkoani dodoma na nje ya dodoma Gifted alikuwa akisikika mara kwa mara kwani alikuwa ni mpenzi wa kutumia media kutoa maoni yake, kuonyesha upendo kwa ndugu na marafiki nk.
Kwaniaba ya Uongozi wa Kipindi cha MICHARAZO TIME toka dodoma fm radio pamoja na Mtandao huu wa ngelangelanews,blogspot.com unatoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki bila kuwasahau wadau wa media kote nchini.
Wapo baadhi ya watu walio toa pole kupitia kurasa zao za facebook kama Maryam Shabani, Fikiri Ramadhani n.k
Lakini pia mtangazaji wa kipindi cha Maisha kiburudani toka Nyemo Fm Sonnatha Abdalah Nduka naye ni miongoni wa watu walio guswa na msiba huo na kupitia ukurasa wake wa facebook ameendika maneno haya.
walllah mpaka sas sijaamin kama haupo nasi tena, #dogo totoo ulikuwa ni shabiki wangu na mfuatiliaji mzuri sana wa kipindi changu cha maisha kiburudani naikumbuka sana text yako uliyonitumia, imekuwa mapema mno jamni naweza kuandika mambo mengi mpaka kukufuru mungu, umetangulia ila sisi tupo nyuma yako mwenyezi mungu akupumzishe kwa amani, poleni wanafamilia @ imma sadala
![]() |
picha ya marehemu Gifted Sadala ENZI ZA UHAI WAKE. |