
LICHA yakuwa anategemea elimu kuwa ni moja kati ya nguzo ambayo inaweza kumbadilisha
www.ngelangelanews.blogspot.com
mtu na kuwa na maisha bora lakini ameamua kugeukia upande wa pili wa maisha na kutumia kipaji chake kuweza kutambulika,kupata kipato pamoja na kusambaza elimu kwa kutumia sanaa.

Anafahamika kama Rachel Njingu au Rachel Bithulo ni mwenyeji wa Mwanza kwasasa ni mwanafunzi wa chuo cha St john dodoma hivi karibuni anatarajia kutoka na filamu mpya aliyocheza na mastaa wakubwa toka Dar es salaam kama MSUNGU, MASENDEE na MZEE JENGUA.

Akizungumza na blog hii amesema kwenye filamu hiyo ambayo inafahamika kama CONFUSIONS na jina ni CLARITHA amecheza kama mhusika mkuu na kuvaa uhusika kama binti mpole na msikivu inakaribia kutoka muda wowote kuanzia hivi sasa na kuongeza watu wakae tayari kuipokea kwani ni filamu nzuri na yakuvutia inayo faa kuangaliwa na watu wa rika zote.
rachel |
Rachel njingu |