Mrembo
Maureen Godfrey katikati akiwa na washindi wa nafasi ya pili Martha
John na mshindi wa tatu Naba Magambo katika picha ya pamoja |
Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2014 Maureen Godfrey akiwapungia mkono wadau wa urembo katika ukumbi wa Highlands usiku wa kuamkia leo baada ya kutangazwa mshindi |
kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gerald Guninita kulia akimpongeza mshindi wa taji la Redds Miss kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2014 Maureen Godfrey baada ya kutawazwa mshindi usiku wa kuamkia leo |
........................................................................................................
ZOEZI la kumsaka Redds Miss kanda ya nyanda za juu kusini limekamilika kwa Redds Miss Njombe 2014 Mrembo Mauren Godfrey kutoka mkoa wa Njombe kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kinyang'anyiro hicho .
Huku mkoa wa Iringa ukiwakilishwa na Martha John aliyekuwa Redds Miss Iringa 2014 na mkoa wa Ruvuma ukiwakilishwa na mrembo wake Naba Magambo ambae ni Redds Miss Ruvuma 2014 kwa ushindi huo warembo hao wa tatu ndio watakaopeperusha bendera ya urembo ya mikoa ya nyanda za juu kusini katika kinyang'anyiro cha kumsaka Redds Miss Tanzania 2014
Katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa na kushuhudiwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gelard Guninita mrembo Maureen aliweza kumpokea taji hilo aliyekuwa Redds Miss Kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2013 Lina Allan ambae alipokea taji hilo mwaka 2011 kutoka kwa Christine Wiliam .
Katika kinyang'anyiro hicho warembo Salome George ,Magreth Tarimo,Naba Magambo,Elizabeth Mussa,Maureen Godfrey,Martha John,Juliana Gilbert,Flaviana Msalila,Faina Salum na Atukuzwe Fabian ndio ambao walifanikiwa kuingia hatua ya kumi bora na kupelekea kuingia katika wakati mgumu zaidi wa kuenguliwa kwa maswali.
Katika hatua hiyo ya kumi bora majaji walilazimika kufanya mchujo na kuwapata watano bora ambao ni Maureen Godfrey,Naba Magambo,Faina Salum,Atukuzwe Fabian na Martha John kabla ya kumpata mshindi wa kwanza hadi tatu kwa njia ya maswali .
Maureen na wenzake wawili waweza kung'ara zaidi katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kujibu maswali na kujieleza zaidi na kupewa baraka za kuiwakilisha kanda ya nyanda za juu kusini katika kinyang'anyiro kama hicho ngazi ya taifa .
Awali mratibu wa mashindano hayo Doss Magambo alisema kuwa mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho atazawadiwa kiasi cha Tsh milioni 1 wakati mshindi wa pili atazawadiwa kiasi cha Tsh 500,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa kiasi cha Tsh 300,000 huku kila mshiriki atapewa kiasi cha Tsh 80,000 kama kifuta jasho zoezi ambalo litafanyika siku moja baada ya shindano