Wananchi mbalimbali wakishangaa mapaja ya Shilole
Maskani ya Mung wee, watoto wadogo wakimshangaa Shilole jinsi.
Na Mwandishi wa Xdeejazy Igunga
Ile
Ziara ya wanamuziki Mad, Queen Durleen na Shilole imeingia doa kufuatia
wananchi wengi kutokufurahishwa na uvaaji aliokuwa ameuvaa Shilole huku
wazee wa Kisukuma na Kinyamwezi kumlani vikali mwanamuziki huyo na
kudai siku akirudi tena huko aje amevaa gauni la sivyo atakiona cha
moto.
Mtonyaji
wetu wa habari hizi ambae alikuwa kwenye msafara wa wasanii hao
aliieleza Xdeejayz kuwa Shilole aliwafanya wakazi hao kushindwa
kufurahia ujio wa wanamuziki hao kutokana na kingu kifupi alichokuwa
amevaa huku sehemu ya mapaja yake ikiwa wazi na watoto kushuhudia nusu
mwili wake jambo ambalo hawajawahi kuona.
Hata
hivyo Shilole ambae amekuwa na kawaida ya kuvaa nusu uchi akiwa stejini
jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakichukizwa nalo na wamekuwa
wakimuonya mara kwa mara kuachana na kuvaa nusu uchi kwa vile mashabiki
wengi wanahitaji burudani na sio kuona maungo ya miili yake, lakini
ameonekan kupuuza.
Xdeejayz
ilimtafuta Shilole kupitia simu yake ya kiganjani ili azungumzie balaa
hilo lililom kuta lakini kwa bahati mbaya hakuweza hadi habari hii
inawafikia wasomaji wetu wenye kiu ya kujua habari na matukio yalijiri
wikiend.