HUU NDIO USAFIRI WA KISASA WA LADY JAYDEE, TAZAMA HAPA - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, January 20, 2014

HUU NDIO USAFIRI WA KISASA WA LADY JAYDEE, TAZAMA HAPA


 
Hahaaaa kweli wanaosema wasanii wabongo si wote wenye njaa kama wengi tuzaniavyo, ni juzijuzi tu hapa msanii Diamond Platnumz kavuta mkoko aina ya Toyota Land cruiser V8. Kitendo hicho Diamond kununua gari hiyo kilikua gumzo sana hasa katika mitandao ya jamii ukizingatia gari hilo ni la bei mbaya.
 Sasa mwanadada Lady Jaydee na e kaamua kujibu mapigo kwa kuonyesha mkoko wake mpya aina ya Range Rover Evoque ambayo nayo pia ni ya bei mkasi lakini bado hajamfikia Diamond. Katika tafutatafuta yetu mdakuzi wa XDEEJAYZ alifanikiwa kupata bei za gari hilo kwa nje ya nchi, ambayo kama ni jipya ni kama dola za kimarekani 45,000 ambazo ni sawa na shilingi za ktanzania milioni 72,495.000 na kama limetumika ni kama dola za kimarekani 42,000ambazo ni sawa na 67,662,000.
Kwa msanii kama Lady Jaydee na Diamond kumiliki magari ya ghalama kama hayo ni uthibitisho tosha kua muziki wa Bongo flava unalipa sana kama wasanii wataamua kufanya mziki kama kazi na si masihara. Ni ukweli usiopingika kua wasanii hawa wawili wameweza kua mfano bora kwa jamii kwani mshiko wanaopata wameutumia kuwekeza katika biashara mbalimbali ambazo zimewafanya kuacha kutegemea pato la muziki peke yake.
 
Timu nzima ya xdeejayz inapenda kuwapongeza wasanii hawa kwa mafanikio waliyopata na kwa kuweza kua mfano wa kuigwa na wasanii wachanga ambao nao siku moja wangependa kua kama wao.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages