Msanii wa muziki aina ya Mduara ambaye asili yake ni Zanzibar A.T Ambaye hivi akribuni ameachia wimbo wake wa Shari amesema anapingana vikali na wasanii wanao lipinga baraza la sanaa la Taifa (BASATA)
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha radio 98.4 Dodoma fm radio kupitia kipindi cha micharazo Time A.T amesema anashangazwa sana na baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakiipinga Basata katika maswala ya kiutendaji na hiyo inatokana na wasanii wengi kujifanya wajuaji.
A.T ameongeza kuwa wasanii wamekuwa wakifnya makosa yakisanaa na kutengeneza mzuki wa chuki halafu wanaanza kugombana na Basata kitu ambacho anasema sio sahihi na ni vyema wakachunguzwa akili zao.
Pamoja na hayo amesema wasanii wamekuwa wakiingiza elimu yao ya darasani bila kutambua kuwa Muziki unaelimu yake tofauti na haifanani kabisa na masuala ya Biology.
Mengineyo amewaomba wasanii kufuata maadili yakikazi nakuacha kuiga tamaduni za nchi nyingine.
@benedict_ngelangela
