
Akizungumza nakipindi cha Micharazo time msanii huyo ambaye amesikika akiimba mistari miwili kwenye wimbo huo amesema watu wengi wanadhani kuwa Ben Pol ndiye ambaye alimwambie aimbe mistari miwili kwa lengo lakuogopa kufunikwa au kubana lakini si kweli kwani aliukuta wimbo huo ukiwa umeshamaliziki tyari na Ben Pol hakuhitaji kuotoa huo wimbo na yeye ni mtu wa kwanza kumshauri autoe wimbo huo.
Wise anasema baada ya Ben Pol kuona ameupenda huo wimbo ndio akamwambia aufanyie jambo lakini kutokana na wimbo kuwa na dakika nyingi alikataa kufanya lolote lakini alilazimishwa na kuamua kufanya kile ambacho aliweza kukifanya kwa muda huo lakini alikuwa amepewa nafasi kubwa yakuingiza mistari na alikaata kutokana na urefu wa ngoma yenyewe.
kwaupande mwingine Wise one amesemabaada yakutoka wimbo huo anashukuru wasanii wakubwa kama Jux na Vanessa kuonesha kuukubali uwezo wake na amepokea hongera nyingi kutoka kwa mashabiki wa muziki.
pamoja na hayo anamshukuru Ben Pol kwakumuweka kwenye wimbo huo ulio kuwa mkubwa kwa muda mfupi.