
sasa siku ya tarehe mwezi wa 3 kumi kupitia moja ya magroup ambayo yanaundwa na wakazi wa dodoma liitwalo pinga undezi lilimweka kikaangoni mwandaaji wa tuzo za nyambago suleish marah ili aweze kuulizwa maswali na kuyajibu moja kwa moja, mjadala huo ulianza rasmi kuanzia saa 6 mchana hadi kumi na mbili jioni.

Mjadala ulianza kwa suleish marah kukaribishwa na maswali yalianza kwa suleish kuyajibu kwa ustadi mkubwa ili kutoa ufafanuzi ya wale walio kuwa wanataka kujua ukweli kuhusu jambo husika, na maswali mengi yalikuwa yakihusu tuzo za nyambago katika maeneo tofauti tofauti.
suleish hakuonesha kuogopa maswali ambayo yalikuwa yanamlenga kwani aliyajibu kwa nguvu na kwa utetezi wa hali ya juu akihakikisha kila mmoja anajua ukweli wa kile kilichokuwa kinaonekana hakikuwa sawa kwenye tuzo hizo.
maswali ambayo yalitawala zaidi ni pamoja na waliopata tuzo walijua mapema kuwa tayari ni washindi?
pia swali ambalo lilikuwa tata ambalo watu walidhani halitajibiwa kiufasaha ni kuwa alihusisha mapenzi na tuzo hizo laikini lilijibiwa na kusema swala la kazi na mapenzi ni vitu viwili tofauti na ni private, swali hilo liliibuka baada ya kusambaa kuwa tuzo ya muigizaji bora wa kike ilihusisha mapenzi ndani yake.
swali lingine ambalo lilizua mjadala ni kuwa kura hazikuhesabiwa na maamuzi binafsi yalichukua nafasi kubwa kitu ambacho suleish alilitolea ufafanuzi na kusema kura zilipigwa na zilihesabiwa na mwenye kipangamizi aende ofisini kwake akuangalie kura na inabidi awe mshiriki ili kuthibitishi alipata kura ngapi.
swali lingine ni kwamba kwanini kamati yake ilijaa watu wenye chuki na upande mwingine pia washkaji wake ndo walijaa, suleish alilijibu na kusema si kweli kwani kila aliye kaa kwenye kamati walikuwa ni watu ambao walitenda haki?
Erick backamaza bila kujua aliko tokea aliandika walaka mrefu na miongoni mwa maneno yake alisema waliopata tuzo wenyewe hawajazifurahia tuzo zao kama wangine walizomewa pindi wakichukua tuzo ndio maana wakati tuzo ya msanii bora wakiume watu walitoka nje.
pia swali lingine ni kwamba suleish marah hamtambui Mogella kama dir wavideo na kama anamtambua kama dir ni kwanini hakuwepo kwenye tuzo, suleish kwa mifano huru na iliyopo alilijibu swali hilo kwa vitendo zaidi kwa kupost picha ya maneno yakionesha kuwa mogella alimtusi na kuzidiss tuzo hizo kuwa alidai ni za kiwaki. pia suleish aliongeza kuwa endapo atamuomba radhi basi atamweka kwenye tuzo hizo.
hayo ni baadhi ya majibu ya suleish marah kwenye group la pinga undezi na ukifuatilia ni kwamba suleish marah licha ya kusemwa bado hajakata tamaa kuhusu kuandaa tuzo hizo.
KIBONZO ni pale rachel njingo na madam key almaarufu kama Joyce key ambao ni waigizaji wa dom movie walionekana kufurahi kikaangoni huku wakichombeza na maneno ya watoto wakike kama unavyo jua, ndipo suleish alipo shindwa kuwavumilia na kuwaambia Rache pamoja na madam key kuwa wanaleta uswahili kama vipi wangeenda kupika hawana cha maana humu ilizua kicheko sana kwani kulikuwa na utani wenye hasira juu yake.
hicho ndo kikaango kilivyo kuwa ndani ya kundi la watsap ambalo linaitwa pinga undezi.