‘BASATA
ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na
ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili
uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini
usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa
maelezo yako‘ – BASATA
‘Baraza
limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho
lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya
katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja
maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha
kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja,
kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote
utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA
source millardayo.
