AIBU YA MWAKA MPYA. MSANII WA BONGO FLEVA MIRROR AZOMEWA MAISHA CLUB DODOMA NA KUKATAZWA KUIMBA. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, January 1, 2015

AIBU YA MWAKA MPYA. MSANII WA BONGO FLEVA MIRROR AZOMEWA MAISHA CLUB DODOMA NA KUKATAZWA KUIMBA.

ishu nzima ilitokea siku ya jana kwenye mkesha wa mwaka mpya mida ya saa 9 usiku wakati baadhi ya watu ambao walijitokeza kwa wingi kwenye club hiyo ya maisha club dodoma wakiendelea kucheza ngoma kali zilizo kuwa zikidondoshwa na ma dj wakali toka club hiyo.

Wakati mambo yakiendelea ndipo dj alipo tangaza surpliz kwa watu kuwa mastaa kibao ndani ya nyumba.na kumtaja mkali wa nyimbo kama one and only na nyimbo kama baby leo mirror ambaye alikuwa amesimama mbele ya dj akitazamwa na watu kibo ambao walikuwa wakiinjoy ngoma za hip hop.
Hali ilikuwa tete baada ya watu kuulizwa kuwa wapo tayari kumsikia mirror akiimba ndipo saut kibao zikikanusha kuwa asiimbe ashuke huku wengine wakipiga buuuuhhhhh!
wakati mashabiki wa muziki wakisema asiimbe ndipo mtu mmoja anae sadikika kuwa ni meneja wa club hiyo alipanda kwa dj kwa hasira akitikisa kidole kuwa asiendeleee kutaja jina la msanii huyo.
Mnyeteshaji wa siri amesema sababu iliyo pelekea mapaka msanii huyo kufanyiwa hivyo ni kutokana wiki iliyo pita maisha club dodoma iliandaa show ambayo ilibidi ipigwe na msanii huyo lakini haikufanyika kutokana na msanii kutolewa na polisi kwa sababu alitangazwa kuwa atakuwepo kwenye show iliyo fanyika matei lounge siku ya mkesha na hakutakiwa kufanya show sehemu yoyote ndio maana viongozi wa club hiyo walichukizwa na alipo onekana siku hiyo walikataa kumpa shavu kwani walipata hasara ya matangazo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages